Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimeshangaa jinsi watu wanavyolichukulia katazo la mifuko ya plastiki Watu wengi kwa kupotoka na kupotosha wanadhani hakutakuwa na hata kitu kimoja kitakachofungwa kwenye mifuko ya plastic. Hiyo sio maana yake, na mtu asikudanganye kuja nyumbani kwako eti anakagua kama una mifuko ya plastic akakuta kuna "packaging" za plastiki akakujia juu au kukudai kitu kidogo.
Katazo la mifuko ya plastiki linahusu hasa maduka (supermarkets)au huduma zinazofungasha vitu unavyonunua katika mifuko ya plastiki, na sio kwa kila kitu
Hizi hapa chini ni baadhi ya bidhaa zitakazoendelea kuwa katika mifuko ya plastiki. Unaweza kuongeza.

- Taulo za kike (pedi)
- Mabunda ya toilet paper
- Six pack za bia
- Baadhi ya sabuni
- Mifuko ya bidhaa maji inayotolewa na maduka ya duty free ya airport
- Karanga za kupakiwa kiwandani
- Chips zilizokwisha kufungwa supermarket
- Mboga mboga kama njegele au karoti zilizokwisha kufungwa supermarket
- Ice unazonunua supermarket
- Mito ya kununua dukani
- Magodoro ya dukani
- Mafiji au TV toka dukani
- Pipi
- Packet za korosha au karanga za kukaanga
- Shati au nguo nyingine za dukani
- Bidhaa za courier kama DHL
- Mifuko ya dry cleaner
- Mikate, maandazi nk ya supermarket au confectionery
- Sukari
- Chumvi
- Nk