Kwa hapa Mwanza nikifanya process za hii Electronic Passport nitaipata baada ya mda gani. Passport inahitajika kabla ya terehe 3 mwezi wa 11.
View attachment 899985
Hakikisha una
1. Kitambulisho cha taifa
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Affirdavit ya mzazi mmoja
4. Barua ya mwaliko au uthibitisho wowote wa safari
5. Application form ambayo utakuwa umeapply online(utalipia 20,000)
6. Barua ya mtendaji wa kijiji/kata kama sio mwajiriwa.
7. Uthibitisho wa shughuli zako unazofanya i.e barua ya mwajiri kama ni mfanyakazi e.t.c
8. Kitambulisho cha kazi kama ni mwajiriwa
9. Barua ya ombi la passport
Wanaweza wakahitaji zaidi kulingana na madhumuni ya safari yako na pia shuguli zako e.t.c
Ingia kwenye hii link utapata kila kitu ikiwemo namna ya kujaza ombi lako online
Online ppt form
Sehemu inayosumbuaga sana ni hapo uhamiaji mkoa kwa maombi ambayo unaombea mkoani ila ukishakamilisha kila kitu na wakapitisha basi ombi lako likishaenda Dar ni chap tu passport yako itatumwa.
Hakikisha wanajua kuwa tarehe unayosafiri imekaribia as watakusaidia uweze kupata kwa haraka kabla ya safari
Ukienda siku ya kwanza kama wakikuambia kuna kitu bado hujakamilisha waambie wakague wakuambie kila ambacho kinamiss maana inawezekana vinamiss vitu vingi ila wakakuambia kimoja tu halafu siku ukirudi tena ndo wanakuambia hicho kingine unajikuta unaenda na kurudi mara nyingi.
Kila kitu utakachotoa kopi i.e cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa e.t.c hakikisha kinathibitishwa(kupigwa muhuri) na mwanasheria/hakimu, sijui kama hili ni lazima lakini mimi waliniambia nikapige muhuri.
Kwa ushauri wangu usiwe mtu wa story nyingi za kuelezea kwa nini huna unapoulizwa document ambayo huna, we nenda kaitafute(utaipataje utajua mwenyewe) usipende sana kuvunja sheria au kutofuata inachosema we ikunje halafu pita, mara nyingi wanachotaka ni kuiona suala la kuwa genuine au sio hawataangalia sana isipokuwa kwa zile document za kitaifa zinazojulikana na kila mtu kama birth certificate na kitambulisho cha taifa. Kumbuka na yeye anapoipeleka kwa mkuu wake inabidi akaanze kuelezea story za kwa nini document fulani haipo na hapo unakuwa unawapa kazi ya ziada kwa hiyo hawapendi sana hizo story.
Kila la heri.