Electrical engineering au Mechanical engineering

Electrical engineering au Mechanical engineering

habari zenuu wakuu.. Mimi ni kijana ambaye nimehtmu form six mwaka huu na nmefnkiwa kupata one ya Tisa kwa masomo ya PCM.. tatizoo languu lipoo kwenye hizo kozi ipiii nifnye ndo first priority kwenye kjazaa na vyuoo vipii ni vizurii kwa hizo kozi mbilii ukizingatiaa mdaa wa kuapply unaklbiaa kuishaa.. Msaada wakuu
Kijara kimsingi electrical engineer jina lake liko juu na ud maksi za kujiunga na electrical ziko juu kuliko mechanical lakini mechanical ni nzuri zaidi. Ukiangalia tanzania inayopanga kuingia kwenye viwanda, mechanical ndio roho ya viwanda. Kiwanda kinaweza kuwa na electrical engineer mmoja au wawili lakini mechanical wataanzia kwenye umeneja, wakuu wa votengo na ukarabati wa mashine mpaka kusimamia uzalishaji. Ukiangalia soko ni kwamba tunakoelekea mechanical itakuwa na soko sana.

Swali zuri, tunaposema "BSc in" hapa unaongelea vyuo vingi kama UDSM,SUA, na vingine vinavyotoa kozi za uhandisi apart from DIT, MUST na arusha...na tunaposema "B.Eng" hii ni kwa vyuo vya ufungi kama DIT MUST, Arusha tech and the alike!!!

"BSc in.." hii ina maana 60% ya masomo itakua ni theory/nadharia wakati 40% ya mafunzo utabase kwenye practicals hawa wanakua vyema sana kwenye analyical skills na designing!

"Bachelor of Eng.." as i said ni kwa vyuo kama DIT, St. Joseph, AIC na MUST...Hawa na base sana kwenye practical katika mafunzo yao na hapa prac inachukua karibu 60% ya mafunzo na theory/ nadharia inachukua 40%!!

Ki uhalisia wote wakimaliza wanajulikana kama ma injinia na wanafanya kazi moja kama wahandisi wa ujenzi/civil engineers!!!
Karibu
Sawaa mkuuu nashukuruu sanaa umenifumbua macho...

Ivi mkuu kuna tofauti gani kati ya fundi (mtu wa veta) na injinia? je ni ipi kazi ya injinia katika ujenzi?? na je fundi wa veta anaweza fanya kazi ya injinia??
ASIKUDANGANYE HUYO.VETA INATOA MWISHO TECHNICIAN LEVEL 1-3 NI FUNDI LAKINI NGAZI YA CHINI SANA VYUO VYA KATI DIT,MIST NK WANATOA KUANZIA LEVEL 4-6 AMBAYO NI ORDINARY DIPLOMA

UNACHOK
Still unadanganya!! unajua kozi ngumu ikoje? wewe unaweza ona mechanical ngumu lakin mwenzako akawa anakushangaa unachosema!

Kwa ushauri tu, unachangia sehemu kama hizi lazima ujue wengi wanasoma unachoandika, so jitahidi kuangalia uandikacho kabla hujapost!
TULIOSOMA TECHNICAL TUNAJUA NA HATA DIT KWENYEWE TUMESHUHUDIA WENGI WAKIKIMBIA ACHA MCHEZO KIJANA LAZIMA TUMWAMBIE UKWELI MWENYEWE ATAJIPIMA KWA UWEZO WAKE.PALE DIT KOZI AMBAZO NI TAITI NI MBILI 2 MECHANICAL NA LABORATARY NA ZIMEPEWA KIPAOMBELE WA UFADHILI ASILIMIA 100

PETROLIUM SIKUSHAURI KWA HAPA TANZANIA NIMEYEYUSHO FIELD NA MALECTURER WENYEWE LABDA UKAISOMEE NJE YA NCHI NA NCHI YETU HAINA UZOEFU WA HIZO KAZI KWAHIYOSIKUSHAURI,ARTCHECTURE AU INTERIOR DESIGN KAMA HUJASOMA UFUNDI AU KAMA KUCHORA HUJUI LIACHE KABISA
Mkuu unasoma kozi gani kati ya hizo?

Huu ndio mwongozo wa degree programmes za engineering zitolewazo hapa kwetu!!
1) Civil engineering
Kwa hapa nyumbani (tanzania) hii kiasi flani ina upana sana katika kujiajiri na kuajiriwa. Ukianzia katika sekta za serikali na binafsi, mashirika mbali mbali ya research yanahitaji hawa watu!! Most likely ukisomea hii kozi uta specialize katika moja hizi fields structural,transport engineering na baadhi ya vyuo wameongeza irrigation na water resources. Nahii ni moja ya kozi mama katika engineering ukiacha mechanical na electrical engineering. kuajiriwa au kujiajiri uwanja upo mkubwa sana!!

2) Irrigation engineering
Kwa hapa kwetu inatolewa na vyuo vitatu tu (SUA na arusha tech,instutute of water dar), hii kozi ni subset ya civil engineering na kwa baadhi ya vyuo wanaijumisha na water resources engineering (Mfano mzuri pale SUA)!! hamna mtu ambaye hajui mabadiliko ya hali ya hewa duniani na madhara yake katioka kilimo na uchumi!! Katika hii kozi utajifunza umwagiliaji, ujenzi, ku design na ku monitor irrigation schemes na structures. Wataalamu wa umwagiliaji wanahitajika sana duniani hasa na makampuni binafsi, bila kusahau kama unataka kuajiriwa na serikali ni rahisi mno na nirahisi kujiari!!

3) Mechanical engineering
Kwa maoni yangu hii inafwatia kwa ubora hapa kwetu!! kama utasomea hii kozi unaweza specialize kwenye energy production, au general... popote ambapo civil engineer yupo huyu lazima awepo!! kazi zao ni katika ujenzi, migodini bila kusahau secta za binafsi na serikali!! uzalishaji wa mashine mbali mbali na kudesign mara nyingi ndio kazi zao!!

4) Electrical and electonics engineering au electrical engineering.
Japo wengi wanasema iko so limited nikimaanisha wao waafanya kazi tanesco tu, hii sio kweli!! hakuna project ambayo inaanzishwa bila hawa watu kuwepo!! migodini, ujezi wa nyumba, bara bara, uzaishaji umeme and so forth kote huko wanapatikana!! na kama ukisomea hii most likely unaweza specialize kwenye power generation, microcomputer, au general electrical!! kwa hapa tanzania bado sana inalipa na ina future nzuri kama utafaulu na kuipenda!! katika hii kozi kama nlivyosema unaweza pia kusomea mambo ya computer kama ukiambua kuspecilize huko..inawezekana!!

5)Agriculture engineering
Kwa hapa nyumbani hii kozi inatolewa SUA kama sikosei na St Joseph nao wameanzisha, nchi sasa imeweka mkazo sana kwenye mambo ya kilimo, na kama unavyoona watu hawa kiasi fulani wapo wachache sana, kama unataka kujiajiri ni rahisi sana na kama kuajiriwa pia haisumbui!! makampuni ya uzalishaji hasa kilimo wanahitaji sana hawa watu, kwenye viwanda nako hawa watu fiti..

6) Petrolium engineering
Hakuna ubishi kwamba gesi imevumbuliwa hapa nyumbani, na kwa msisitizo hii kozi imeanza fundishwa kwenye vyuo kama UDSM (imeanza mwaka huu) na UDOM!! ni kozi nzuri na future yake ni nzuri, ila kama unataka kujiajiri nadhani haitakua rahisi kiasi flani na mara kwa mara unaweza ajiriwa na serikali!! changamoto nyingine ni kwamba, katika field hii ya gesi hasa hapa bongo makampuni mengi yenye tenda ni ya nje na mara nyingi wanakuja na wataalamu wao(simaanishi wataalam wa ndani hawaajiriwi), sasa hapa mbongo kupata kazi kiasi flani inaweza kua ngumu!!

7) Chemical engineering
Mara nyingi hawa watu wanabase sana kwenye viwanda na uzalishaji(processing) kwa ujumla. na kwa hapa tanzania inatolewa na vyuo kama viwili kama sikosei(UDSM na SUA), bado hawa watu wanahitajika sana na ni choice nzuri. Kwa mtazamo wangu hawa watu ni ngumu kidogo kujiajiri(simaanishi haiwezekani kijiajiri), labda kama unauwezo ukaanzisha kiwanda chako...

8) Computer engineering, Software engineering
Kuliko ukasomee computer science (kama unataka kusomea engineering) ni bora ukasomea moja ya hizo mbili. kwa hapa bongo inakaugumu flai kupata kazi katika serikali ila ni rahisi sana kujiajiri hasa kama consultant engineer. tukianza na compurer engineering wana deal sana na hardware na kiasi flani computer science imemezwa na hii, na kwa baadh ya vyuo ukifika mwaka wa tatu unaweza ukaspecilize katika software engineering!! software engineering, on the other hand, kwa hapa tz inatolea na UDOM pekee, bado sana watu wake wanahitajika sana katika sekta binafsi na serikali!!

9) Architecture
Japo inaonekana kama sio field ya engineering, ila believe me hamna project inafanywa bila uwepo wa architect na yeye mara nyingi ndiye anadesign let say nyumba then anamkabidhi structural engineer, wataalamu wake wapo wachache hilo halina ubishi, kama unajiamini ni mbunifu(and ofcourse to be an engineer/architect you must be creative) hii field nzuri sana hasa kwa hapa bongo!! ni rahisi sana kujiajiri na inasemekana (haya ni maneno ya watu) hata ukiwa mwanafunzi hasa mwaka wa nne na tano unaweza ukawa unapiga pesa mtaani kama uko smart enough!!!

USHAURI

Kama ndio unachagua vyuo, ni vyema ukachagua vyuo ambavyo havina usumbufu hasa wa kutoa pesa za malazi kwa wanafunzi. Ni vyema ukaangalia vyuo vikongwe vya serikali mara nyingi havina usumbufu.

Hamna kitu kizuri kama kufanya kazi au kitu unachopenda toka moyoni mwako bila kulazimishwa na mtu!! kwa field yoyote utayoenda hakikisha unaenda sio kwa sababu inalipa ua utapata tittle mtaani ila kwa sababu unaipenda toka moyoni!! kumbuka changamoto zipo anzia shuleni (ku-sup) mpaka makazini...ila kama umeenda kwasababu unaipenda kamwe hutatishwa na changamoto hizo!!!

Kusoma kozi kwasababu umefaulu tu haitoshi soma kozi kwasababu unaipenda. Kumbuka ni kitu kizuri kama kutimiza ndoto zako maishani!! Ukifanikiwa maliza usisahau kujisajili kama proffesional engineer ili utambulike ndani na nje....na kama unaswali usisite kuuliza..

Karibuni sana Uhandisini , na kila heri katika kufanya choices za vyuo na kozi...

Upepo wa pesa (G.Eng.)

mambo vp jamaa!ikiwa mwnfnz kapata c tatu mbili phy na

ikiwa mwnfnz wa olevel kapata c tatu mbili phy na bio moja kisw na d ya kemia f ya math afanyaje ili asome dip ya electrical engineer.

Maganga Mkweli najua wewe ni mhandisi wa umeme... embu njoo utoe mchango wako huku
kwa ufaulu wake mlimani/coet anapata MECH kwa vyuo vingine kama DIT anapata UMEME/ELECT
MECH inazo fursa nyingi hasa hii dunia ya automation
ELECT ndio usiseme
kwa mlimani na kurecommend jaza MECH ila sijajua matokeo yako ya OLEVEL
karibu ulimwengu wa wahandisii

kwa ufaulu wake mlimani/coet anapata MECH kwa vyuo vingine kama DIT anapata UMEME/ELECT
MECH inazo fursa nyingi hasa hii dunia ya automation
ELECT ndio usiseme
kwa mlimani na kurecommend jaza MECH ila sijajua matokeo yako ya OLEVEL
karibu ulimwengu wa wahandisii
Umepotea kabisa JF mkuu....i remember those days tulikua tunachagua vyuo...infact kwa sasa tushakua wahandisi.... karibu tena jukwaani mkuu!!!

Aisee kila la heri mkuu, naipenda shule ila sio hio shule unayotaka kwenda kuianza wewe mkuu...Maisha hayajawa promising kiasi hicho hapa nchini!

Mimi ni Accountant. Dogo chagua unachopenda from your heart, zote ziko poa. Na mungu atakusimamia mbeleni. Amiin

kwa ufaulu wake mlimani/coet anapata MECH kwa vyuo vingine kama DIT anapata UMEME/ELECT
MECH inazo fursa nyingi hasa hii dunia ya automation
ELECT ndio usiseme
kwa mlimani na kurecommend jaza MECH ila sijajua matokeo yako ya OLEVEL
karibu ulimwengu wa wahandisii
O level nlipataa one ya kumi na NNE kaka..physics nlikuwa na B+ Chemistry nlkuwa na B+ na Mathematics A(hyo ni kutokna na grade za mwaka ule 2013)...Pia mkuu naomba unisaidie na hilii nmejazaa electrical kam first priority kwa UDSM na Second priority nmejzaa Mechanical UDSm.. Vipii nkikosa first kna uwezknoo nkpta hiyo ya pili

MECHANICAL ENGENEERING INATOLEWA DIT NIA NGUMU KIASI KWAMBA SPONSORS NI ASILIMIA MIA ILA MNAWEZA KUMALIZA WATANO KATI YA 40.KAMA UMESOMA ENGINEERING SCIENCE OLEVEL UNAWEZA KUJUA PICHA HALISI YA MOTION NA MACHINE TOPIC HIZI ZINAEXPAND BALAA
Mkuu acha kumtisha dogo

dogo kwa kua unatoka six ni bora ukapige degree ya umeme tu..

O level nlipataa one ya kumi na NNE kaka..physics nlikuwa na B+ Chemistry nlkuwa na B+ na Mathematics A(hyo ni kutokna na grade za mwaka ule 2013)...Pia mkuu naomba unisaidie na hilii nmejazaa electrical kam first priority kwa UDSM na Second priority nmejzaa Mechanical UDSm.. Vipii nkikosa first kna uwezknoo nkpta hiyo ya pili
utaratibu wa selection wanaotumia ni wanaojaza selection namba moja ndio wanachukulia kulingana na vigezo vya ufaulu. utachukuliwa chaguo la pili kama una vigezo vya hiyo kozi hiyo uwe umewapita wale waliojaza chagua hiyo kozi kama chaguo la kwanza .. kwa sasa naona umeme UDSM ina ushindani mkubwa sana tofauti na Mech maoni yangu ni bora ungeweka Mech kama first option , utaweza kusoma option kozi za umeme /kama electromechanical ...

utaratibu wa selection wanaotumia ni wanaojaza selection namba moja ndio wanachukulia kulingana na vigezo vya ufaulu. utachukuliwa chaguo la pili kama una vigezo vya hiyo kozi hiyo uwe umewapita wale waliojaza chagua hiyo kozi kama chaguo la kwanza .. kwa sasa naona umeme UDSM ina ushindani mkubwa sana tofauti na Mech maoni yangu ni bora ungeweka Mech kama first option , utaweza kusoma option kozi za umeme /kama electromechanical ...
Sawaa Mkuuu nashukuru sanaaa..

Back
Top Bottom