Hawa electricious eel wapo hata kwenye mabwawa mengi tu Dar mfano pale mkwajuni kwa chini mpaka kule jangwani wanapatikana, ubungo - kijitonyama - mwananyamala kuja mpaka kinondoni lile bwawa wanapatikana sana. Mimi kama mimi binafsi nimeshawavua kwa kwa ndoano, na naweza kusema hatukujua kama ana uwezo wa kuzalisha umeme kwasababu mara nyingi tukishamtoa mtoni kwa ndoano tulikuwa tunawapiga kichwani ili wafe tukiamini baada ya dakika chache wanageuka nyoka kumbe in unknown reason tulikuwa tunaepuka balaa la umeme wake dah. Mungu alitunusulu kweli kweli