Inasikitisha sana kuona kila siku tunapoteza ndugu zetu kutokana na uzembe wa wenzetu tuliowapa dhamana ya kutulinda. Watu wamekubuhu katika kutuhujumu mpaka wamefikia hapo, hili suala linauma sana tena sana maana kila unapoona ajali ujue hapo maskin wanaongezeka. Mtu leo alikua na nguvu(viongo) za kufanya kazi(kujitafutia chakula) lakini ikishatokea ajali anaanza kua tegemezi. Hali ni mbaya kupita kiasi na kama itaendelea hivi ipo siku watanzania wanaopoteza ndugu zao kwa uzembe wa baadhi ya wau wataihitaji vichwa vya hao watu pamoja na familia zao.