Ekerege na TBS, hongera kwa mauwaji. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ekerege na TBS, hongera kwa mauwaji.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sikonge, May 2, 2012.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama unamfahamu mfanyakazi yeyote wa TBS, basi inabidi ukampe HONGERA zake kwa kuwa hela wanazozipata kwa kuruhusu matairi feki ya magari, watu wanazidi kufa na kuumia.

  Tunajua mmetengeneza hela nyingi sana kwa kuyaruhusu. Pia nyie wafanyabiashara mliyoyaleta, tunafahamu kuwa hamna hata huruma kwa binadamu wenzenu ila ipo siku na nyie mtalipa. Malipo ni hapahapa duniani.

   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mods, naomba hii muiache kwanza hapa kwa uda ili hawa Wafanyabiashara na TBS wakiongozwa na huyo EKEREGE, waone jinsi watu wanavyokufa na kupata majeruhi ya milele kwa uzembe wao ukiongozwa na uroho wa Rushwa.

  Hapa hujawaongelea wale wanaokufa na Kansa kwenye mahospital. Too bad.

  [​IMG]
   
 3. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana kuona kila siku tunapoteza ndugu zetu kutokana na uzembe wa wenzetu tuliowapa dhamana ya kutulinda. Watu wamekubuhu katika kutuhujumu mpaka wamefikia hapo, hili suala linauma sana tena sana maana kila unapoona ajali ujue hapo maskin wanaongezeka. Mtu leo alikua na nguvu(viongo) za kufanya kazi(kujitafutia chakula) lakini ikishatokea ajali anaanza kua tegemezi. Hali ni mbaya kupita kiasi na kama itaendelea hivi ipo siku watanzania wanaopoteza ndugu zao kwa uzembe wa baadhi ya wau wataihitaji vichwa vya hao watu pamoja na familia zao.
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ekelege sasa imetoshaa
   
Loading...