Ekari 100 za mashamba ya miwa, zateketea kwa moto Zanzibar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
c66e811fe342642ff56ed8ee4c6f7e8f.jpg


Hekari zaidi ya 100 za mashamba ya Miwa zimeteketea kwa moto katika kile ambacho wamiliki wa mashamba hayo wamedai ni njama za makusdi zinazofanywa na watu au kikundi maalum.

Tukio hilo la kuteketeza kwa mashamba hayo ya Miwa ambayo yako katika kiwanda cha sukari kiliko Mahonda mkoa wa kaskazini Unguja ambacho kinaendeshwa na wawekzaji kutoka India ambapo hili ni tukio la tano kutokozea katika kipndi cha miezi miwili na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Akizungumza na vyombo vya habari afisa utumishi wa kiwanda hicho ambacho kinara kwa kuzalisha sukari hapa Zanzibar Bashiir Mohmaed amesema moto huo ni njama zinazofanywa na watu au kikundi kwa maksudi huku wao wakishindwa kujua sababu za mashamba hayo ambayo yalikuwa tayari kwa kuvuna Miwa na kuanza uzalishaji.

Mkuu huyo wa utumishi amesema kiwanda hicho ambacho kinatoa ajira kwa zaidi ya watu 300 kinalazimika kufungwa kutokana na hali hiyo amabyo amesema ni hasara kwa wawekazaji na wananchi wa Zanzibar.

Hata hivyo mmoja ya mlinzi wa kiwnada hicho mzee Saidi Mussa ambaye yuko kwa miaka mingi kiwandani hapo amesema iko haja ya pande zote kukaa pamoja na kutafakari nini tatizo la mara kwa mara kuwepo kwa moto.

Katika ajali hiyo ya moto ya mwisho ilishuhudiwa na viongozi wa seriklai akiwemo mkuu wa mkoa wa kaskazini ambaye alikuwepo kuangalia tatizo hilo huku kamnada wa polisi wa mkoa wa kaskazini Mohmaed Msangi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema polisi wanawashikilia watu wawili na uchunguzi bado unaendelea
 
Kumbe zanzibar kuna kiwanda cha sukari?? Anyway hapo lazima chanzo ni maslahi tu si bure. Wakae chini wajitafakari vizuri. Kama watashindwa kufikia suruhu, panaweza ibuka mzozo mzito ambao unaweza fanya kiwanda hicho kisitembee kwa ufasaha
 
Inawezekana ikawa ni mambo ya siasa? Mtu mwenye kuchoma ekari 100 au hoteli lazima mbinu zake ni very effective, ana mtaji na yuko organised maana hawezi kufanya peke yake
 
Mimi sijmauelewa huyo mlinzi,wakae waongee pande mbili anamaana gani?upande mmoja uongozi wa kiwanda na upande wa pili ni UPI???!!!

+Wafanyakazi??
+Wakazi wa eneo lililopo karibu na kiwanda/mashamba ya miwa??

RUCCI
 
Mimi sijmauelewa huyo mlinzi,wakae waongee pande mbili anamaana gani?upande mmoja uongozi wa kiwanda na upande wa pili ni UPI???!!!

+Wafanyakazi??
+Wakazi wa eneo lililopo karibu na kiwanda/mashamba ya miwa??

RUCCI
Ndo maana mie nkahisi ni maslahi tu. Na hapo washa sema wahindi. Hawa watu wanakatabia ka kuchangia chama kikuu.
 
Back
Top Bottom