Eh! Jamani kumbe haya mambo bado yapo njii hii....!!!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eh! Jamani kumbe haya mambo bado yapo njii hii....!!!??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Oct 14, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wakati Tanzania leo ikiadhimisha miaka 11 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa mkoani kigoma ikiambatana na na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru. Habari nilizozipata ni kuwa meneja wa SIDO mkoani kigoma aliyefahamika kwa jina la Daniel Njowelo amewekwa rumande kwa amri ya mkuu wa wilaya ya kigoma Bw. John Mongella.

  Sababu ya Bw. Mongella kumuweka ndani meneja huyo wa SIDO ni kuwa kuna miradi ya vikundi vidogo vidogo inayokadiriwa kufikia Shilingi bilioni 7 ilitarajiwa kuzinduliwa. Jiwe la msingi la miradi hiyo inasemekana kuwa lilijengwa na SIDO ili siku ya kuwasili mwenge hapo kigoma basi uzinduzi ufanyike ambapo Raisi kikwete alitarajiwa kufanya uzinduzi huo. Kituko ni kuwa jiwe la msingi lilitakiwa kufunikwa kwa kitambaa ili siku ya ufunguzi mkuu wa kaya anafunua kitambaa kuashiria uzinduzi huo badala yake jiwe hilo la msingi likawa liko wazi tu hadi siku ya leo ambapo mkuu wa kaya akazindia hiyo miradi kwa kufuta vumbi tu.

  Jambo hilo halikufanyika na alipotafutwa meneja huyo wa SIDO alikutwa akiwa katika bar moja akipata yale maji ya pale ilala bila wasiwasi wowote na kujikuta akisombwa msobemsobe hadi polisi.
   
 2. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Sheria ya mkuu wa wilaya au mkoa kumweka mtu ndani bado ipo, tatizo hapo wana-abuse badala kuitumia sheria katika mazingira ambayo yanakubalika mfano kuwaweka ndani wakimbizi wanaoleta vurugu nchini.
  Suala ya mkuu wa wilaya huko kigoma kumweka ndani sababu ya jiwe la msingi, ni tatizo na makosa ya Mongella mwenyewe sababu alitakiwa kuwa na kamati ya maandalizi ambayo yeye angekuwa mwenyekiti na kuwa na checklist ambayo ingekakikisha kila kitu kimekamilika mapema kabla ya siku mbili.
  Hapa inaonekana walikuwa hawana team ya kufanyakazi ila kila mmoja alikuwa anafanya kivyake vyake.
   
Loading...