EFD ni sawa lakini hazitoshi..

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,874
4,277
Migomo ya EFD inayoendelea sehemu tofauti za nchi inatokana na wafanyabiashara wengi kutokuwa na elimu ya kutosha na kukosa uzalendo. Wengi ni wakwepaji wa kodi na hawaweki mahesabu yao wazo. Tatizo siyo bei ya machine hizo, ingawa bei bado ni kubwa ukilinganisha na device zenyewe. Kihalahi kabisa hizi efd ni sawa tu na calculator za kawaida zenye memory kubwa na uwezo wa kukonect kwenye gsm network. Bei yake inatakiwa isizidi laki 2.

Hata hivyo TRA inabidi wabuni mbinu zaidi. Kwa sasa hakuna incentive yeyote kwa mtu kudai risiti halali. Kwa mfano ni watu wangapi tukiweka mafuta kwenye gari tunadai risiti halali. Ya kazi gani.

Juzi kati hapa nimenunu mzigo wa milioni mbili nikapewa risiti ya laki 6. Jamaa akaniambia kama nikikupa risiti ya mil 2 itabidi ulipe mil 2.2. Kwakuwa sikuwa na muda wa kubishana naye na vili vile sikuwa na incentive yeyote ilibidi niondoke tu. Kwani hata nikipapanda ni sawa na kuweka tone la maji kwenye bahari.

TRA wanatakiwa watengeneze incentive kwa wanunuaji kudai risiti halali kulingana na malipo waliyofanya.

Njia moja wapo ya kusaidia ni kuanzisha mfumo wa tax return. Watu wote wawe na TIN unapienda kununua kitu inatamka TIN yako na jina linatokea kwenye risiti. Then kuwe na uwezo wa kutrack ni kiasi gani cha kodi ulicholopa. Kwa mfano nikiingia kwenye website ya TRA niweze kuprint statement ya ulipaji wangu wa kodi. Kuanzia PAYE, VAT n.k. Mwisho wa mwaka TRA warudishe kiwango flani cha kodi kama 10% hivi. Hii itanisababisha nidai risiti kila ninapofanya manunuzi kwani itaniongezea kwenye returns zangu za mwisho wa mwaka. Hivyo kabla ya kununua nitataka nihakikishiwe kupata risiti halali. Tukifanya hivi automatically wafanya biashara watatoa risiti halali. Kwa sasa kodi inayopotea ni zaidi ya 10% itskayorudishwa.

Fedha za returns zaweza kurudishwa cash kupitia account au vocha unayoweza kutumia kulipia huduma au kodi nyingine za serikski kama kulipia road license, school fees etc.
 
Back
Top Bottom