Eeeh mwanamke

Eeeh mwanamke

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,678
Ewe mwanamke, kama mumeo anaingia hadi ndani ya nyumba huku akiwa amebeba mzigo wowote, iwe bahasha, mfuko nk, wakati umemuona na umeshindwa kumpokea, anza kujitasmini upya.

Ew mwanamke, kama unalala hadi mumeo anaamka asubuhi na kwenda kuoga, anajiandaa kutoka kwenda kazini ukiwa bado umelala, fikiria upya nafasi yako katika ndoa.

Ewe mwanamke, kama mumeo anahitaji tendo la ndoa, unashindwa kumpatia kwa sababu za kutojisikia au kizingizio cha kuumwa, ukitafutiwa msaidizi usilalamike.

Ewe mwanamke, kama unamnyima mumeo haki yake ya tendo la ndoa na kufanya tendo hilo kama sehemu ya adhabu pindi mnapokwazana, siku zako zinahesabika.

Ewe mwanamke, kama hutuoi nafasi ya kumsikiliza mumeo pindi anapozungumza na ukayafanya mazungumzo hayo kuwa sehemu majibishano, anza upya mumeo atachelewa kurudi nyumbani kama atapata wanaomsikiliza huko.

Ewe mwanamke, kama unatabia ya kupuuzia kila unachoambiwa na mumeo ukidhani anachokwambia amaanishi, tambua inamuumiza ndani kwa ndani na mwisho wa siku atashindwa kutoa nafasi kwako ya kukushirikisha au kukushauri chochote.

Ewe mwanamke, kama unakaa na marafiki zako na kuongea udhaifu wa mumeo ukidhani utapata tiba na ufumbuzi, tambua hao marafiki zako ndio watakao kucheka pindi utakapo baki single mather kwa uvivu wako wa kufikiria.

Ewe mwanamke, kama umeamua kuutoa mwili wako sada kwa mwanaume ambaye si halali yako kwa lengo la kutafuta kufukishwa kileleni au tamaa zako za pesa, tambua kwamba bado hujajitambua, swala la kufikishwa kileleni unatakiwa ukae na mumeo mlizungumze ili kulitafutia ufumbuzi wa kina na sio kwenda kutafuta maradhi nje au mimba za bahati mbaya.

Ewe mwanamke, kama kazi zote za nyumbani unamuachia house girl kwa kudhani kwamba utamlipa mwisho wa mwezi, usishangae siku atakapokuwa mama mwenye nyumba au mke mwenzio.

Ewe mwanamke, kama una tabia ya kuropoka ovyo, kumdharau mumeo, kupenda ligi na mabishano angali bado upo kwenye ndoa yako, tambua kwamba mumeo anakuvumilia tu lakini kichwani mwake anafikiria kuwa huna vigezo vya kuwa wife material, anajuta kwanini alikupa hiyo nafasi ya kuwa mke.
____________________________
Hizi mambo zitakuvunjia ndoa dia
 
Nipo na wife baada ya kusoma amesonya nafikir ujumbe umemfikia
 
Back
Top Bottom