Eee Mungu...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eee Mungu......

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mohammed Shossi, Aug 24, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  [FONT=&quot]Rabbi uloumba mbingu, Ukaumba na dunia
  Nasi kwetu walimwengu, Dini ukatushushia
  Nini letu fungu, Sisi ulotuwekea

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kutwa kucha twakuasi, Maovi kuyavamia
  Tena bila ya kuasi, Mengi tunakusudia
  Mola haiwi basi, Waja kwako twarejea

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Muombozi wetu nani, Kwayo tunokutendea
  Ya Illahi ya Manani, Wapi tutakimbilia
  Tutaingia motoni, Kama hujatupokea

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Twakuomba Rahmani, Waja wako twatubia
  Tunataka samahani, Kila tulokutendea
  Sisi sote duniani, Na waliyotangulia[/FONT]
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndiye weye peke yako, Mwengine hapatikani
  Twataka shifaa yako, Akhera na duniani.
  Kama si rehema zako, sisi sote mashakani.
   
 3. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  sisi sote mashakani, bila ya rehema yako
  hatokei duniani, wa juu zaidi yako
  wote insi na majini, wote ni viumbe wako
  tusamehe waumini, tuipate pepo yako

  tuipate pepo yako, tusamehe waumini
  tupe na rehema zako, akhera na duniani
  na kila lo zuri kwako, kwetu wala situkhini
  sisi sote waja wako, tusamehe ya Mannani.
   
Loading...