Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Ushiriki wa wabunge wa upinzani ndani ya Bunge unaonekana kuendelea kuwa finyu kutokana na hamahama, huku halmashauri zikizidi kupoteza idadi kubwa ya madiwani na wenyeviti walioingia madarakani kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wengi wanaona hizi ni dalili nzuri kwa siasa za Tanzania hasa mustakabali wa vyama vya upinzania ambavyo hakuna shaka vimekuwa na mchango katika maendeleo ya Taifa tangu siasa za ushindani ziliporejeshwa mwaka 1992