bakuza
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 492
- 104
Aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa wakati akimnadi mgombea wa CCM Sioi Sumari hapo jana eneo la Patandi alijinadi kuwa mjadala wa matizo ya ardhi,maji na umeme huko Arumeru umefungwa kwa sababu CCM imetabua na kusikia matatizo yao ktk uchaguzi huu mdogo wa ubunge wa Arumeru Mashariki.Ninachojiuliza hapo ni hiki:
- Tatizo la aridhi,maji na umeme Arumeru lilidumu kabla ya uhuru na baada ya uhuru mwaka 1961 hadi leo na CCM ndiyo ipo madarakani kwa kipindi hicho chote.Je hawakuwahi kuliona tatizo mpaka ktk uchaguzi mdogo.
- Lowassa aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, na Maendeleo ya Makazi. katika serikali ya Rais Ally Hassan Mwinyi kati ya mwaka 1993 hadi 1995.je tatizo la ardhi hakuliona?
- Lowasa amekuwa Waziri wa Maji kwa miaka mitano chini ya serikali ya Rais Mkapa kati ya 2000 na 2005,lakini hakujishugulisha na hilo tatizo hata kidogo au anataka tuamini hakuliona kipindi hicho au harikumhusu?
- Pia huyu huyu Lowassa amekuwa Waziri Mkuu kipindi cha Jakaya Kikwete kabla ya kutimka sababu ya kukosa uadilifu kwa kufisadi mali ya Umma.
- Zimefanyika jumla chaguzi kumi za ubunge huko Arumeru kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia je ktk chaguzi hizo walikuwa wanahaidi na wanatatua kero zipi wakati hata barabara hakuna?
