kali KENYATTA
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 288
- 166
Kuna dhana mbalimbali zimejengeka juu ya mtangaza nia ndugu Edward Lowassa. Dhana hizo kwa ufupi ni kama uwezo wa kuchukua maamuzi magumu ambayo kimsingi hayawekwi wazi ni yapi. Pia kuna dhana ya uchapa kazi ambayo imekua ikitetewa zaidi na watu wa kambi yake kwa kutolea mifano isiyojitosheleza kimaudhui. Vilevile, kabla na wakati wa mchakato mzima wa kuitangaza safari ya matumaini, tumeshuhudia vitendo mbali mbali vinavyoashiria jeuri yake pamoja na wanaomzunguka dhidi ya mamlaka ya chama na serikali. Kwa ufupi ni mambo mengi yametokea na yataendelea kutokea kuelekea ukingoni mwa mchakato mzima wa kumsaka mrithi wa Jakaya Kikwete.
Nikiwa kama mtanzania kijana mwenye matumaini makubwa na Tanzania ijayo, nakumbwa na mashaka sana na ushabiki unaoendelea juu ya dhana ya maamuzi magumu ya ndugu Edward Lowassa. Mara nyingi nimemsikia akizungumzia dhana hii bila kufafanua maamuzi magumu yanalenga shabaha gani katika kuondokana na umaskini uliokithiri hapa nchini. Kwa mfano, alipokua akitangaza nia ya kuomba ridhaa ya wana CCM kugombea kiti cha urais mkoani Arusha, kauli ya maamuzi magumu ilisababisha uwanja wa Amri Abeid kulindima kwa shangwe za hali ya juu. Mimi binafsi nilibaki nimeduaa nisijue maana halisi ya shangwe hizi. Kwa maoni yangu, nadhani hayo ndio mazingira yanayopelekea watu kuamini kwamba ndugu Edward Lowassa ananunua watu wanaohudhuria mikatano yake. Ni mtu aliyenunuliwa au mwenye uwezo mdogo wa kufikiri anayeweza kushabikia vitu asivyoviamini.
Nadhani shabaha ya dhana ya uchapakazi inalenga kuonyesha ni kwa jinsi gani ndugu Edward Lowassa anafaa kua kiongozi wetu kwa sasa kuliko wakati wowote ule. Kwa maana nyingine ni kutaka kuonyesha kwamba watanzania hawawezi kuhamasika kufanya kazi mpaka wapate rais mchapa kazi kweli kweli. Utata mwingine unaibuka ni kwa jinsi gani tunajua kupima uchapakazi wa mtu, je ni kukesha ukifanya kazi yenye matokeo hafifu au ni kufanya kazi kwa ufanisi? Rafiki zangu wengi wanamzungumzia Edward Lowassa kama mchapakazi asiye na mfano, kwa kiingereza tuseme kwamba, "he is a job addict".
Kimsingi dhana hii ya uchapakazi ni sehemu tu ya vigezo vingi vya kiongozi bora. Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi mwenye maono anayeweza kulihamasisha taifa kuamini kwamba maendeleo ya kweli yataletwa na watanzania wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Hatuhitaji kiongozi wa staili ya Edward Lowassa ambaye wakati wa uongozi wake kama waziri mkuu aliwatisha watendaji wake badala ya kuwahamasisha wafanye kazi kwa bidii na maarifa.
Suala tata zaidi juu ya mtia nia huyu ni tabia ya watu wanaomzunguka. Ni kana kwamba uchaguzi huu unapitia vita kali kati ya kundi la wenye kipato kisicho halali dhidi ya wanaojipambanua kua wazalendo wa kweli. Ni kama vile wale tunaowajua kwamba ni mafisadi wanataka kusimamisha uongozi wa kifisadi ili kulinda maslahi yao. Na upande mwingine wa shilling ni kwamba kundi la wazalendo limejipanga kuingia madarakani kwa nia moja kubwa, nayo ni kuwashughulikia mafisadi. Hii ni vita kubwa sana na bahati mbaya wahanga ni maskini wale wale wanaoshabikia mambo wasiyoyajua.
Nachelea kusema kwamba, Edward Lowassa amezungukwa na watu wanaotiliwa shaka na taifa. Wengi wao ni watuhumiwa wa ukiukwaji wa maadili ambayo ni msingi muhimu wa uongozi. Katika mazingira kama haya, Edward Lowassa hawezi kukwepa kuitwa si mwadilifu ikiwa rafiki zake si waadilifu.
Nitaendela..