Edward Lowassa, awapa mitaji vijana walioondoka naye CCM

zahra omari

Member
Mar 2, 2015
21
5
Katika kuonyesha Utu na kujali Vijana wake, aliekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA kupitia Mwavuli wa UKAWA Kamanda Edward Lowassa amewapa Mitaji Vijana wake waliohama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vijana hawa wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Chuo Cha IFM na Mwenyekiti wa 4UMovement Taifa Hemedi Ali na Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Rorya na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa UVCCM Wilaya Sango Kasera walienda kumuomba Kamanda Lowassa Awasaidie kupats Mtaji wa kujiimarisha Kiuchumi, kwani hali ya Vijana wengi ni mbaya na wanalalamika huku wakijuta kujiingiza Siasa za Upinzani.

Kama kawaida yake Kamanda Lowassa aliwajibu kwa Kifupi na Kiutekelezaji zaidi, "undeni Company na nitawasaidia kupata Capital ila muunde network na wengine huko Mikoani wapate Salam Zangu, Come up with a good Company Propassal that will have branches every were, This Company will kill CCM 2020".

Kwa sasa Vijana wa Lowassa waliondoka CCM wanakula Bata Tu, ila Taarifa za uhakika ni kuwa kampuni hii ni Mtandao wa kuingoa CCM 2020.

Vijana wanaoshughulikia Usajili wa Kampuni hii ni Ernest Nyoni, Fadhili Fabian Ngajilo, Fred Mushi na Richard Lowassa. Na lengo lingine la Mtandao huu ni kuiteka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Katika Uchaguzi wa Chama ujao Vijana hawa wachangamkie nafasi Nyeti, Alisikika Mmoja wa Vigogo wa Mradi huu ambaye Jina lake la Utani ni Bilionea Mangi alisema kwa lafudhi ya Kichaga "2020 Mtoto hatumwi Dukani, CCM na Magufuli wao wataisoma Namba, na Moto Utaanza katika Uchaguzi wa Chama 2019'.
Nimeamini Lowassa ni kichwa na kila Senti yake anaitumia vyema, Sasa ninaelewa ni kwa nini anapenda Kusema anaichukia sana Umaskini.

NB; KAMPUNI HII IKIFANYA KAZI KAMA ILIVYOPANGWA CCM BYEE BYEE 2020 BY KACHERO MBOBEZI AKA SCO......
 

Attachments

  • download (2).jpg
    download (2).jpg
    11.1 KB · Views: 83
Duh!
Sisiemu bye bye 2020??? Hii ya Magufuli?? Itabidi EL atununue watz wote Na ahakikishe anatusimamia ktk ballot box tunatick jina lake, uzi huu ni useless!
 
Africa na Tanzania inahitaji watu intelligent, wabunifu.... Wanaojituma zaidi na wenye kujali tija na ufanisi kuliko nguvu nyingi isiyo na tija!!

Lowassa ndani ya mwaka mmoja alimu outshine JK kiasi kwamba akajengewa chuki na wivu... Wanafiki na wadandiaji waliokosa vyeo na fursa wakaanza uchonganishi hadi kuwatenganisha na JK! Ni lowassa huyu aliyesimamia bila woga ujenzi wa shule za kata nchi mzima japo walikuwepo waliopinga na kubeza!! Miaka miwili baada tangu aondoke hazikupata msukumo tena!! Zikageuka day care centres!!!

UDOM ni mawazo na uthubutu wa Lowassa!!

Itafika mahali muda utatuambia ni jinsi gani majungu... Chuki...visasi na husda zinavyoimaliza nchi hii yenye neema tele!!
 
Lowassa kwa mtaji huo unipati mm. Mbele kwa mbele na JPM, tunajenga uchumi wa nchi ya tanzania sio wanachadema tu.
 
Kwahiyo hiyo kampuni ndio itapiga kura kwa niaba ya watz, au inatengeneza pesa kwa ajili ya kununua kura?! Kwa staili hii 2020 hamtaisoma tena namba tu, bali hata maandishi ya mlangoni mtayakariri!!:D
 
LOWASSA si alisema hana pesa??? Kazipata wapi? WACHA WAMLE TU URAIS ASAHAU KABISA!!!
 
sema anawarudishia pesa zao maana ndiyo pesa alizoiba kwa watanzania.. arejeshe ziishe.
 
LOWASSA ANA SIFA ZOTE ZA KIONGOZI BORA.

Tofauti na huyu mwingine anayewanyanyasa wanyonge na kuwaacha kina January Makamba,Chenge na kina Charles Kitwanga...Lowasaa yeye ana uchungu na wananchi wadogo.
 
Ni wazo zuri kwa vijana wetu kupata msaada wa kuendesha maisha na kujishughulisha na biashara.

Lakini huyu Lowasa ana pesa kiasi gani? Jee hizo pesa zimelipiwa kodi na ni halali? Au hii ni mbinu za kinga ya jipu lake kutotumbuliwa.
 
Back
Top Bottom