UKAWA itisheni press conference na mtoe elimu ya kupiga kura kwa wananchi. Asiende mtu mmoja kama Mbatia bali siku hiyo jopo zima liwepo ili kuweka uzito na iwe live.
Vinginevyo, kama wadau walivyosema hapo juu, uwezekano wa dotCom, bodaboda, na wapiga kura wengine ambao hawana experience kuharibu kura kwa kuweka X kwa wagombea wengine ni mkubwa mno ukizingatia uchaguzi huu ndio wa kwanza wa aina yake kwa watanzania kujitokeza kwa maelfu kupiga kura. Hawana experience na Tume haitaki kuwaelimisha, wasaidieni.