Ed Woodward, Jose Mourinho na msemo wa "Kwenye miti hakuna wajenzi"

Mtu Kati

Member
Jan 12, 2017
33
54
Tangia Mourinho amepewa jukumu la kuinoa klabu ya Manchester United msimu huu wa 2018/2019 utakuwa ni msimu wake wa tatu na tayari amekwishafanya usajili wa wachezaji 11 hadi sasa ambao wanne kati yao Paul Pogba Henrikh Mkhitaryan Eric Bailly na Zlatan Ibrahimovich aliwasajili katika msimu wake wa kwanza tu wa 2016/2017 akiwa kama kocha wa mashetani hao wa Old Trafford.

Wakati ule Mourinho anaichukua timu aliainisha maeneo ambayo angependa yaboreshwe na aliweka wazi kuwa anahitaji beki wa kati kiungo wa kati winger pamoja na striker ambao aliwapata tena wote wakiwa ni wachezaji wa kaliba ya dunia lakini licha ya kupewa kile alichohitaji timu ilimaliza msimamo wa ligi ikiwa nje ya zile nafasi nne za juu ahsante kwa ubingwa wa Europa league ambao ulimsaidia kupata nafasi ya kucheza champions league msimu uliofuatia sasa basi kwa hapa sio Ed Woodward wala familia ya Glazer wanaostahili lawama kwa kushindwa kupata ubingwa wa EPL ambao ndio kiu kubwa kwasasa kwa wapenzi wa Man utd.

Baada ya matokeo yale mabaya na yasiyoridhisha ndani ya uwanja hatimaye Mourinho aliingia katika msimu wake wa pili akiwa kocha wa Manutd huku akiahidi kurejesha furaha katika nyuso za wapenzi wengi wa klabu hii kongwe waliotapakaa kote ulimwenguni kwa kuwapa taji la ligi kuu walilolikosa kwa miaka minne mfululizo, kama ilivyokuwa kwa msimu uliotangulia Mourinho aliomba board yake inayoongozwa na mwana mahesabu Ed Woodward impatie wachezaji katika maeneo yaleyale kama ambavyo aliomba kupatiwa katika msimu uliomalizika na safari hii Victor lindelof beki wa kati kutokea katika klabu ya Benfica na timu ya taifa ya Sweden alisajiliwa huku.

Mbelgiji Romelu Lukaku akisajiliwa kwa pesa ndefu kutoka katika klabu ya Everton lakini pia kiungo Nemanja Matic aliingizwa kikosini kutoka kwa mahasimu wao Chelsea na huku tukiarifiwa kuwa mchezaji pekee ambaye Mourinho alimtaka na hakupatikana alikuwa ni winger Ivan Perisic kutokea katika klabu ya Inter Milan ya nchini Italia na hii ilitokana na klabu yake kukataa kumuuza kwani tuliona ofa kadhaa zikikataliwa na vigogo hao wa soka la Italia hivyo bado kwa hili pia hauwezi kutoa lawama kwa uongozi wa juu wa klabu ya Manchester united ambao kwa kiasi kikubwa walijitahidi kutimiza mahitaji ya mwalimu sambamba na hilo katika kumridhisha Mourinho.

Mwezi January walifanya usajili mwingine mkubwa kwa kumsajili Alexis Sanchez chini ya pua ya mahasimu wao kutokea jiji moja la Manchester klabu ya Manchester City ambayo ilikuwa imekaribia kuinasa saini yake Maisha yanataka nini zaidi ya hiki licha ya board kumpa nguvu na msuli wa maana katika usajili wa wachezaji bado klabu ya Manchester United iliendelea kufanya vibaya katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na hii ni kutokana na mbinu mbovu na za kizamani za mwalimu José Mourinho ambaye licha ya kusajili wachezaji wake wanane ambao aliwapendekeza mwenyewe lakini bado aliendelea kuwatumia wachezaji walewale aliowarithi kutoka kwa watangulizi wake.

Hebu pata picha umetumia zaidi ya £70M kusajili walinzi wa kati tena waliosajiliwa kwa mapendekezo yako lakini bado unaopt kucheza na Smalling na Jones kama beki zako za kati sio hilo tu lakini pia unamuweka bench mchezaji ghari zaidi katika historia ya ligi kuu ya Uingereza na kumpatia nafasi Scott Mctominay mchezaji wa hadhi ya bench katika timu nyingi za Championship licha ya haya yote lakini bado mwalimu Mourinho anapiga kelele na kulialia kuwa board ya klabu haimpi support katika suala la usajili wa wachezaji.

Msimu huu klabu imesajili tena kiungo mwingine Fred kutoka kwa Shakhter Donetski mabingwa wa ligi kuu ya Ukraine hivyo kufanya kiasi cha €200M kutumika kusajili wachezaji watatu wa eneo la kiungo pekee kipi board ifanye ili Mourinho aache kulialia?? Licha ya kusajili mabeki wa katikati kwa hela nyingi bado anataka board impatie £65M amsajili Harry Maguire mchezaji aliyeng'ara katika mechi 6 pekee za kombe la dunia huyu ndio Jose Mourinho.

Kuhusiana na Guardiola kurithi kikosi imara zaidi ya Mourinho na kuendelea kusajili wachezaji wengine hili siliafiki hata kidogo kwa kutazama jambo moja sana la msingi. Ukijaribu kuitazma Manchester City ndani ya misimu hii miwili iliyopita kocha Pep Guardiola amepitisha fagio la nguvu sana katika kikosi cha Manchester City akiamini wachezaji wengi aliowarithi kutoka kwa mwalimu Manuel Pellegrine walikuwa ni wakawaida sana na hivyo ndivyo ilivyo kwasababu ukiondoa Wachezaji wanne tu ambao ni Fernandinho De Bruyne Raheem Sterling na Sergio Aguero.

Wachezaji waliosalia wote wameshaondoka kutoka katika kile kikosi ambacho kilirithiwa na Pep Guardiola so hapa tunapata picha ya wachezaji kama Jesus Navas Bacary Sagna Gael Clichy Kolalov Yaya Toure Fernando Ihenacho Mangala Joe Hart Dzeko Jovetic Demichelis na wengine ambao walipewa ahsante kwa kushiriki na Guardiola so kusema Mourinho aliikuta ManUtd iko vibaya sio kweli bali yeye ndiye anayezidi kuitia ubovu huu tunaouona leo.

Kuhusu issue ya kutuambia Manutd chini ya Ed Woodward imekuwa na tatizo katika kufanya usajili hili nalo sikubalini nalo kwasababu tangia Woodward avae viatu vya utendaji mkuu wa shughuli za Manutd kutoka kwa nguli David Gil tumeona Manutd ikifanya sajili nyingi kubwa na za bei mbaya kupita wakati wowote ule katika historia ya klabu. Makocha wote wa Manutd tayari wameishi katika kivuli cha Ferguson hivyo hawawezi kukosa kulalama huyo David Moyes alipewa pesa awasajili Gareth Bale Toni Kroos na Ander Herrera badala yake akachagua kumsajili Maroune Fellaini ambaye alifanya nae kazi katika klabu yake ya awali ya Eveeton.

Louis Van Gaal na yeye kama ilivyo kwa David Moyes nae alipewa pesa afanye usajili wa wachezaji anaowataka matokeo yake akamsajili Di Maria na kuwa anampanga katika nafasi ya ulinzi eneo la kushoto uharibifu wa kipaji wa kiwango kilichopitiliza alimsajili Radamel Falcao moja ya washambuliaji bora kabisa kwa wakati ule akaishia kumgeuza kuwa mshambuliaji mbovu zaidi kwa wakati ule then tunakaa tunalaumu kuwa Ed Woodward hatoi back up ya kutosha na hajui namna ya kufanya handling ya transfer na kusahau kuwa kwenye miti hapana wajenzi fedha iliyoko Manutd angekutana nayo Guardiola leo stori zisingekuwa hizi.

#ArticleGuru
 
Mashabiki wa Man utd Chunguzeni vizuri sisi Arsenal tulikuja kugundua kua Wenger anabet na hua anaikataa Arsenal.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom