Economics 101: Laffer Curve

Economics 101: Laffer Curve

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Mchumi Arthur Laffer aliyezaliwa 1940, na kusoma katika vyuo vinavyosifika kwa uchumi kama Stanford na Yale, ambaye pia amehudumu kama Professor katika Chuo chenye shule nzuri ya Uchumi University of Chicago, alileta muonekano mzuri wa kuhusu kodi.

Laffer anasema ukiwatoza watu sana kodi, unapunguza mapato ya serikali. Kwa maana ukitoza watu hela zaidi watakuwa wanakwepa kodi zaidi au wanaacha kufanya kazi, suala linalosababisha mapato ya kodi kupungua. Aidha anajua kabisa ukitoza 0% ya kodi pia mapato ya serikali yanapungua.
1763467060573.png

Rais baada ya kuapisha wateule wake amewaambia mawaziri kuwa kutakuwa na shida ya kupata fedha kutoka nje kutokana na kilichotokea wakati wa uchaguzi. Kwa kusema hayo ametoa wito kutumia vyanzo vya ndani. Kwa uzoefu wangu, watu wanapowaza kodi huwa wanawaza vyanzo vipya, hali itakayopelekea raia kuumia na kodi zitakazotozwa.

Nimeona niweke uzi huu wa basic economic principles ili mawaziri wasianze kuleta kodi ya kichwa nk, bali watumie mawazo ambayo yameshatolewa maeneo mengi kuhusu kuboresha ukusanyaji kwenye vyanzo vilivyopo.

Matatizo ya kodi nchini yako kwenye makundi mawili, High income earners na Informal sector. High Income earners wanahitaji sheria madhubuti zisizoweka mianya ya kukwepa kodi, na informal sector inahitaji "Nudges" ili kodi zilipwe kwa uzuri.

Kuhusu "Nudging" informal sector wapo watanzania wengi ambao wameshaliandikia suala hilo ni suala tu la kugoogle na kusoma au kuita mjadala na wasomi hawa ili washauri.

Namalizia kwa kusema, ni kweli hatutapata hela, na vyanzo vya ndani viziwe chanzo cha kumminya mtanzania.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom