East African Community na umoja wa mashaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

East African Community na umoja wa mashaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, Sep 26, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  KAMA MMOJA WETU ANAWEZA KUMHUJUMU MWEZAKE NAMNA HII NINI MAANA YA UMOHA HUU,NINI FAIDA YAKE KAMA SI KUAMBUZANA MATATIZO.

  Muungano wa Ulaya umeamua kusitisha msaada kwa Rwanda.Uamuzi wa Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
  Taarifa zinazohusiana Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuwatoza kodi wananchi. Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.Lakini Rwanda imeendelea kukana madai hayo.
  Umoja wa Mataifa unafanya mkutano na baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano huo ni swala la mgogoro huo Mashariki mwa Congo. Mapema mwezi Julai Marekani ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda.Msaada wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la Rwanda, lakini hatua hiyo ilitoa ishara kubwa. Kwa kukata msaada huo, Marekani ni kama ilikuwa inasema "tunaamini ripoti kuwa Rwanda inatibua usalama wa kanda hiyo kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Congo".

  Mwezi Juni ,Umoja wa Mataifa ulikabidhi ripoti kwa Baraza la Usalama, ambayo ilisema ina ushahidi mzito kuwa Rwanda inalipatia kundi la M23, wapiganaji na zana, na kurahisisha makamanda wao wakubwa kusafiri na kuvuka mpaka baina ya Congo na Rwanda.

  Uasi huo ulianza mwezi wa Aprili, wakati wanajeshi mia kadha wa jeshi la Congo walipofanya ghasia. Uasi huo uliongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa kivita. Nayo serikali ya Uholanzi ilisitisha msaada wa dola milioni 6.15 kwa Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na madai hayo ingawa baadaye ilianza tena kutoa msaada kwa nchi hiyo baada ya serikali ya Rwanda kuahidi kushirikiana na kukomesha vita hivyo.
   
 2. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,400
  Likes Received: 10,518
  Trophy Points: 280
  Haueleweki
   
 3. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  sieleweki wapi?
   
 4. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Nchi ndogo km Rwanda inatishia usalama wa taifa kubwa km Congo kwa kusapoti waasi,wakati huo huo serikali yenye jeshi kubwa inatishiwa na kikundi kidogo cha wa M23,hivi ni kweli au ni usanii wa mataifa makubwa kama tulivyozoea ufadhili wao kwa vikundi mbali mbali vya waasi kwa manufaa ya nchi zao,sina uhakika sana na uhusika wa Rwanda kwenye hii current crisis,rather kwenye ule mgogoro wa 1998-2003 uliotatuliwa na SADC
   
Loading...