mchambawima1
JF-Expert Member
- Oct 16, 2014
- 2,487
- 738
ah, sasa wewe unawaonea huruma wanyarwanda, je wabongo halisi waliyotimuliwa utasemaje, huku wahindi na hao waarabu unaosema wanapeta? mi namuonea huruma na namuombea kwa Mungu Mh. Magufuri afanikiwe kuokoa jahazi! kwani mambo mengine yananizidi uwezo, hebu tazama...Hapo sipati picha murutongore, kweli ndugu zetu Watanzania ni shughuli. Eti unasema baadhi ya hao waliofukuzwa Tanzania walikua wamezaliwa humo, na wameishi zaidi ya miaka 45 na wana certificate of naturalization. Huo si unyama jameni? Mtu hata kama asili yake Marekani ila amezaliwa nchi yako na kuishi hiyo miaka yote, ukimpeleka Marekani lazima atachanganyikiwa, hata kama kuzuri kivipi.
Ndio mimi nilishakataa katakata haya mambo ya kuingiliana, siwezi ishi nchi ya watu wala kuruhusu watoto wangu wasomee huko. Nimepata fursa nyingi sana za viwanja huko Tanzania, haswa pale Kigamboni lakini siwezi thubutu aki ya nani hii noma. Ingia, piga kazi zako halafu geuza, Wahindi na Waarabu ndio huwa nawashangaa, wamefaulu kununua viwanja, kujenga na kuishi bila kujali ubaguzi wa aina yoyote ile. Lakini mweusi noma, eti Kagame na Kikwete wanakosana kidogo kwa maneno, hapo mnaanza kuwafukuza wote kisa na asili ya Rwanda.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzanians-mistaken-for-illegal-immigrants.html