EAC nchi zashindwa michango!

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,633
7,912
Kama kichwa cha habari, kinavyosomeka hapo juu kuhusu ukata mkubwa kwenye jumuiya ya EAC.

Hadi sasa hivi tunavyoelekea katika uchaguzi wa bunge la EAC mwezi kesho tarahe 4/4/2017.

Taarifa zilizopo ni kuwa hali ni tete kwa sababu nchi wanachama wameshindwa kuchangia bajeti zao kwa wakati ambapo hadi sasa hivi, ni Uganda imetoa 91% ikifuatiwa na Kenya, kisha Rwanda, hapo nchi yetu Tanzania, ni ya nne imechangia asilimia 35% na hali ni ya msiba kwa Burundi ambayo haijachangia hata senti moja.

Hiyo ni taarifa kutoka kwa wabunge wa bunge la EAC ambao wamesema hata malipo yao hayajafanyika.

Swali kwetu sote na hata kwa wakuu wetu wa hizi nchi:-

Je , kuna umuhimu wa kuwa na hii jumuiya !?

Au tuivunje na kuunganisha nchi zote katika jumuiya mojawapo kwa mfano, wote wa EAC tujiunge huko SADC ili kuondoa tatizo la kuchangia jumuiya nyingi?

Na hili ni kwa sababu, hapo EAC kila nchi ni mwanachama wa zaidi ya jumuiya moja.

Mfano: Tanzania, iko EAC na SADC, Uganda, EAC na IGAD, na nchi zote zilizobakia zote nazo zina jumuiya zingine ambazo nazo ni wanachama.


Wajuvi wa mambo watusadie kujadili.

Chanzo: BBC Swahili.
 
Back
Top Bottom