E Mwl Nyerere amka wanao tunaangamia!

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
WanaJF hakika ninayafikiria baadhi ya mambo yanayotendeka humu nchini sasa nikiwakumbuka marehemu mwl J Kambarage Nyerere,E Moringe Sokoine na wengine waliokuwa na mapenzi mema na taifa letu hakika machozi yananitoka.Pia najifananisha na watoto waliofiwa na wazazi wao wamebaki yatima malezi wanayoyapata sasa ni ya manyanyaso tupu.Hivi kweli Tanzania ya sasa kweli ndiyo ile niliyoiona kipindi kile cha vita ya Idi amini wananchi walikuwa na mapenzi mema na taifa lao pia kwa majeshi yao ya ulinzi,wananchi walikuwa wanachangishana vyakula,ngombe, damu kwa waliokuwa wanaumia vitani tofauti na sasa hadi inafikia wananchi wanajenga uadui na serikali yao E mungu waongoze viongozi wa nchi hii warudi katika misingi waliyoiacha waasisi wa taifa letu ambao waliikata misingi mibovu ya matabaka ya walio nacho na wasiokuwa nacho.
 
Back
Top Bottom