Ni wiki ya tatu sasa kuna baadhi ya maeneo ndani ya viunga vya jiji la Dodoma hayana maji kabisa. Mnyetishaji wangu anaiambia maeneo kama Chidachi, kinyambwa, itega na kielekea Michese hayana maji kabisa licha ya kuahidiwa kuwa yatapatikana.
Mnyetishaji huyu anazidi kunidodosolea kuwa Duwasa wanasema wana shida ya umeme kwenye mashine zao shida ambayo hawajafafanua kuwa ni nini hasa.
Lakini wakati wanachi wanaendelea kukosa maji kuna maeneo hasa yale ambayo viongozi na wabunge wanaishi yameendelea kupata maji kwa mass 24 siku 7 zote za wiki. Duwasa wameamua kufanya hivi ili kuficha ukweli kwamba sasa hivi kuna Tatizo kubwa la maji linaloukabili mji wa Dodoma. Waziri wa maji tafadhali tembelea Duwasa maana watu wanapata tabu hapo makao makuu ya nchi
Mkuu achana na mnyetishaji ingia idara ya maji wewe mwenyewe utapata jibu kuhus kwenye iyo sababu yao ya umeme maana siku hiz ukanjanja mwingi hadi wanakela Dadek,,, mim nikionaga miyeyusho napiga simu ad kw mkurugenz