'Duwanzi' - wetu ni popo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Duwanzi' - wetu ni popo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Feb 7, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Leo ni mnyama kesho ni ndege.

  Yuko wapi mwa Jf mwenye mtiririko atutengenezee documentary kuwajuza watz chronology kamilifu ya kuhusu Dowans.
  Naamini itatusaidia kwa kukeep track ya hii movie na kutafakari kinachoendelea behind the scene Ngoja nijaribu kuanza- kwa kumbukumbu zangu (MTANIKOSOA na KUBORESHA) ilianza hivi:

  1. Taarifa kuhusu hukumu ya ICC kuwa tanesco iwalipe dowans sh 185 bn/=

  2. Kelele za hapa na pale zikihoji uhalali wa kumlipa aliyerithi mkataba hewa. Watz wakataka msimamo wa serikali

  3. Pinda akasema tunaipitia ile hukumu na japo tunajua inaumiza ikibidi kulipa hatuna ujanja tutalipa.

  4. AG akaingia na kutangaza kuwa ameipitia kikamilifu na akaridhika kuwa iko sawa na inabidi ilipwe. Akasisitiza jitihada zozote za kukata rufaa/hazipo kwani ni kujisumbua
  (HUU NDIYO USHAURI WAKE WA KITAALAM KWA SERIKALI) nakumbuka hakuonesha kuwa na shaka na kipengele chochote cha hukumu hiyo!

  5. Kelele zikaanza upya kufuatia statement ya Ag na hasa aliponesha kufunga mjadala (ambao kwa macho ya maleimen ulikuwa bado mbichi sana) ama kweli huu ndio weledi wa the learned bros and sis... Kelele za awamu hii zikaelekezwa zaidi kwenye umiliki wa Dowans. Mara yupo mara hayupo, yuko uarabuni, yuko kariakoo, yuko ..., yote hii haiingi akilini kwani tunajua duniani kote (isipokua bongo) kuna utaratibu wa kisheria wakufanya 'company search' na kwa muda mfupi sana na kwa malipo kidunchu 'token' ukapata jibu.

  6. Waziri wa Nishati na madini Ngeleja akaja na 'Msimamo wa Serikali' kwanza akataja wale aliowaita wamiliki wa Dowanzi ambao ., na pia kama AG akasisitiza kulipa ni lazima, tena haraka. Ajabu yeye akazungumzia kulipa sh 94 bn/= bila hata kutupa mkokotoo uliotutoa sh 185 bn alizoafiki AG kuja kwa zake sh 94bn.

  7. Kelele zikazidi nyingi zikipinga ukweli juu ya usiri wake. Pia anavyoingia au kuhusika RA. Baadhi ya wapiganaji wakatutonya msidanyanyike hao wamiliki ni wakutengeneza na hukumu imejengwa kisanii kutupora. Wakaandamwa kuwa wamekosa sana kwani kuna 'collective responsibility' sijui kama hii dhana inatumika hata katika wizi. Kama ni hivyo wasemetu kauli mbiu yao ni (SSS): “Together we STAND, together we STEAL and together we SINK'.

  8. Matamko yakaanza: Mara Uvccm ? mara ….na kupokelewa na matamko zaidi …?

  9. Kamati kuu ya chama ikakaa sijui walisema nini kwani hat alichoeleza Chiligati wenzake wanampinga pamoja na kuwa JK anakubaliana naye ..
  10. Mama yetu Maria Nyerere akashangaa serikali kutaka kulipa dowans
  11.?
  12. ?
  13. Jk anakiri hata yeye anajua Richmond ni hewa...Serikali inajaribu kuona jinsi ya kutomlipa Dowans

  Ili mradi tunachanganywa…

  Nawasilisha
  :embarrassed:
   
Loading...