Mkuu gfsonwin,nimefurahi kukusoma kwa mara nyingine tena,nafarijika sana...
Unajua kwa nchi za wenzetu,hizi tunazoziita dunia ya kwanza huwa wanavipaombele vya taifa ambavyo huwa haviyumbishwi na siasa zao,
Kwa mfano Bill clinton(Democrat) alipoiacha nchi ile kwa George Bush(Republican) na kisha G Bush kuondoka na kuiacha nchi hiyo hiyo tena Barack Obama wa Democrat hawatofautiani katika kusimamia vipaombele vya taifa lao,
Ima iwe ni uchumi,usalama na kadhalika,
Huku kwetu inashangaza sana,kila anaekuja huwa anakuja na sera zake na ajenda zake na kuacha kuangalia lipi ni la msingi na la kitaifa la kuliendeleza na lipi la kulipa muda,suala la Mtwara Corridor JK kalipuuza ili hali suala hili lilikuwa na umuhimu kitaifa na si kikanda,mwezangu yeye nadhan kaja kulichukulia kuwa sual hili chinga Mkapa alifanya katika kutafuta kujikomba na kuwasaidia wamachinga wenzake na sio taifa na ndio kwa maana hatushangai kwa yeye kulipuuza na kuhamishia akili yake kwao bagamoyo kwa kipindi hiki cha miaka miwili ilyobakia,najiuilza sana huyo rais ajaye atakuwa na misimamo ipi??sijajua kama atatokea CCM au la,
Ila kikubwa kinachonishangaza ni kwamba wenzetu hawa nchi zao hizi huwa wanabadilishana badilishana,
Msimu huu chama hiki,msimu ujao chama kingine,lakini linapokuja suala la national interests siasa na ubabaisha huwekwa kando na kufanya kazi,sasa hawa jamaa hupokezana vijiti wenyewe kwa wenywe,sasa najiuliza tatizo linatokea wapi??
Kwanini huyu anakuja kulipindisha la yule hali ya kuwa wote ni wamoja??na huwa wote kwenye meza moja za maamuz kichama na kiserikali??
Inashangaza sana kwa kweli...
Kabisa gfsonwin, uko sahihi. Hakuna hicho kitu kinachoitwa priorities katika nchi hii wala kufuatwa utaalam. Nikiunga mkono juu ya uimarishwaji wa kitaasisi, nadhani vyombo viwili vilitakiwa viundwe na vitambulike na Katiba. 1. National Economic Advisory Council(NEAC, Baraza la Taifa la Ushauri wa kiuchumi), na liwe huru na wajumbe wake watokane na merits na maadili na lisiwe biased na upande wowote, pamoja na majukumu ya kuishauri nchi katika masuala ya kiuchumi lakini pia Baraza hili liwe linapitia na kupitisha Ilani za vyama vyote vya siasa ili kubaini kama ziko in line na vipaumbele vya nchi bila kutoka katika mstari. Chombo cha pili ni Baraza la Taifa la majadiliano ya mikataba (National Council on International Negotiation) likichukua nafasi pia ya GNT ambayo imeonekana kujali personal interests zaidi. Vyombo hivi viwe huru, na viwe wazi katika masuala yote ya vipaumbele na mikataba ili kuepusha wanasiasa kutekeleza mipango ya maendeleo unaotokana na utashi, ukabila, ukanda, udini au any personal interests. Sikubaliani na mfumo wa majadiliano unaotumika hivi sasa ambapo mambo yakiharibika hakuna wa kumkamata, na majadiliano yanahusisha watu either wasio na uwezo wa kujadiliana au wenye maslahi binafsi. Kinyume chake, maamuzi makubwa ya nchi hii yataendelea kufanywa na watu wenye upeo duni na kuleta maisha duni daima-dawamu. Nami pia niwashukuru Mchambuzi na Nguruvi3, kwa muda mrefu nimekuwa nikijifunza mengi sana kwa watu hawa hasa namna wanavyoweka pembeni ushabiki wa kisiasa katika mijadala yao. Mungu awalinde na azidi kuwaongoza.Karibu sana kaka yangu THE BIG SHOW.
Naomba sasa nijibu hoja yako na ya ndugu yangu , kaka yangu Zinedine kama ifuatavyo;
Nimeona hoja iliyoibuka katika mabandiko yenu #278 na #280 ni kwamba HATUNA NATIONAL PRIORITIES ambazo zinatakiwa ziwe AMONG THE FIRST PRIORITIES kwa pesident candidate. na baraza lake la mawaziri.
Kwangu mimi naona sasa umefika wakati wananchi tuamue kwenye katiba hii mpya of which sijui kama itakuwepo kweli ama la kwamba among other things, ni kwamba rais anayechaguliwa lazima ahakikishe kwamba anafwata national interest na hizi zinatakiwa zipangwe na Katibu mkuu Kiongozi akishirikiana na watu wa sera na mipango ya ofisi yake.
hapa nina assume kwamba huyu CHIEF PERMANENT SECRETARY sio mwanachama wa chama chochote cha siasa na huyu tunaweza kumfkukuza na kumshtaki iwapo atakwenda kinyume na matakwa ya katiba yetu.
Binafsi kuna siku nilishiriki kwenye mjadala wa rasimu mpya ya katiba, nilishangazwa sana kuona pale hatukujadili mambo kama haya ila tulijadili sijui eti katiba iwe inasema mwanaume/mwanamke badala ya mwananchi...........ghhhhhhhhhhhhh nilikasirika sana, yaani sijui na wale waliokuja walitudororesha na nini......................
mara tunajadili ooh! kwenye katiba tuondoe ulazima wa mtu kuimba wimbo wa taifa, kwasabbau uko biased kwa mtu asiye mwamini Mungu.............. mimi niliboreka sana nikajiondokea manake niliona sina cha kuongea. Kumbe kuna mambo ya msingi kama haya ambayo tunatakiwa tuyajadili kwa kina kabisa.
napenda sana niwashukuru Zinedine, THE BIG SHOW Nguruvi3 na Mchambuzi kwa kunishirikisha katika mjadala huu na kujibu hoja zangu. Lakini pia napenda niwasisitize kwamba we are the voices of soo many people tusikae kimya lets talk am sure ipo siku tutasikika tu.
Binafsi sijapata muda mzuri wa kujadili rasimu ya katiba ila when given chance ningependa sana nishiriki mjadala wenu wa aina hii.
once again thanks.
.
Leo tunawaacha Wamtwara kwasababu tuliwaacha wa Nyamongo, Geita na Bulyamhulu.
Kesho tutawaacha wa Mchuchuma na Kiwira kwasababu tuna uzoefu wa kuwaacha wenzetu.
Kikundi cha watu wachache kinazidi kutumaliza eti kusimamia haki ya kujua haki yako ni uchochezi, eti ni ukorofi, udini na upinzani.
Tukifanikiwa kugoma kugawanywa na kusimamia haki hapo tutakuwa na jibu la swali la Zinedine.
Nguruvi3 rejea bandiko lako #279 , umenieleza kitu cha ajabu sana toka kukua kwangu sijawah kukiskia. How comes mradi mkubwa kama huu hauna EIA?? JE NEMC, na ofisi ya makamu wa rais mazingira wanacho cha kujitetea??
WHO knows kutattokea nini as a result?? je inamana serikali yetu licha ya kwamba ni mshirika wa makubaliano ya utunzaji wa mazingira duniani na kila mwaka inalipa membership fee na ikakubali kuwepo na penalties kwa kila mshirika atakayekiuka maswala ya utunzaji mazingira lakini bado yenyewe inashindwa kutekeleza makubaliano??
je serikali unless inatuficha lakini kwa jinsi nijuavyo mimi ni kwamba kwa kutokuwa na EIA kwenye mradi kunapelekea taifa kulipa kiasi kikubwa sana cha fedha kama faini sasa hili lingeweza kuepukika tu.
tizama swala la KIHANSI TOADS lilivyoigharimu nchi hii fedha nyingi sana na bado mpaka leo mtu nayewalea vyura hawa hapa UDSM analipwa pesa nyingi sana ishu ni kwamba hakukuwa na EIA sasa je bado serikali inarudia makosa haya haya??
angalia mradi wa kakobe na mpaka leo umeme bado hauwaki licha ya kwamba serikali imezika na kusmamisha mabilion ya hela pale lakini wapi je hatujifunzi??
sasa jamani tunaze sisi wananchi kuamka na kulazimisha mabadiliko ya kweli kwenye hili taifa. kama mradi wa gesi huu hauna EIA hauna sera ya gesi je tunafanya drilling ya nini??
ngoja ni kwambie kwenye nchi walizoendelea ungekuta mradi kama huu watu wamesha study in real cost benefit anaylsis. watu wangekwisha kujua mradi utaigharimu nchi sh ngapi kama matumizi ya mwezi na nchi ingepeta sh ngapi kama mapato yake. tungekwisha kuproject gesi bila wataalam ingegharimu expert importation kwa kiasi gani, lkin pia tungeweza kuinvest kwenye human resource wakati hawa wagen wakiwa kwenye contract.
unajua kuna mambo mengi sana ndani ya hii nchi yanafanyika kisanii sana, mfano mwingine ni huu unakuta donors wamekuja hapa na bonge la mradi na mapesa yao, lkn cha ajabu unakuta mradi unaanza mbeleni unakutana na mapungufu ndipo eti wanasema watu waende short courses sasa najiuliza huo muda wakiwa short courses kazi za mradi wanamwachia nani?? je kwann wataalam wako wasiwe updated kila mara na sio kipindi cha miradi tu?? leo hii muulize procument officer yyte guidelines procurement za WB/IDA uone atakavyo kushangaa. lakini serikali itasubiri hadi IDA walete mradi ndipo wapeleke wataalam wakati vitu kama hivi hawa wangetakiwa wapewe since wakiwa vyuoni na mwajiri alazimishwe atleast kila baada ya miaka 3 amfanyie training huyu mtumish ili awe aware na standards za kimataifa.
utashangaa sana kuona vitu kama M&E eti ni watumish wa serikali wa muda mrefu lkn bado hawawez na ni managers wa taasisi unajiuliza hivi huyu meneja anafanyaje kazi zake?? hivi kweli inamaana sisi hatuna standars??
ukitaka kichekesho nenda kwa internal auditors utashangaa yaani zaid ya kujua audit za kitanzania hawana ujuzi wowote kuhusu international auditing unashangaa mpaka uje mradi mkubwa watu waanze kuona ugumu ndipo waseme tumwombe huyu donor tupeleke watu short course sasa kama ni short course kwann usipeleke kabla hao watu wako??
mimi narudia tena kusema kama wataalam wa RISK MANAGEMENT, FINANCE &AUDIT, M&E, PROCUREMENT,GAS DRILLIN ENGINEERING, MECHANICAL ENGINEERING, ENVIROMENT protection EXPERTS, NA CIVIL ENGINEERING hawajaanza kufikiriwa na hii serikali basi huu mradi utakuwa ni wa maangamizi kwa taifa as hakuna kitakacho kuwa kinafanyika zaid ya hasara tu. tena uje uskie bomba la gesi limepasuka ama sijui limeibwa.
Ogah ,gfsonwin hatuna upungufu wa taarifa wala watalaam. Tunaupungufu wa viongozi na uongozi.Ogah;6938615]Mkuu wengine tunaalikwa/tunaombwa kwenye nchi za watu tukatoe ushauri kuhusu mazingira.....na tunapotoa maoni kwa serikali husika wananzingatia......tena mijadala ya mazingira huwa ni ya wazi sana.......wananchi hushirikishwa kwa sana.......kuanzia kuelimishwa mpaka kutoa maamuzi.......
Kwa nchi mbali mbali ambazo nimepita......NGO za mazingira ziko so ACTIVE.....vitu haviendi kiholela holela....hata kama serikali imeamua.....na kama vinaharibu mazingira basi ndio mwisho wa mradi........Ndiyo tuilaumu NEMC.....lakini kusema ukweli sijawahi kusikia NGO ya mazingira huko nyumbani iliyo ACTIVE.....tunategemea kusikia kelele za Dr. Terezya peke yake....HAWEZI....na yeye keshasema...unfortunately!!
kuna nchi zingine zina Marine National Parks sijui kama kwetu sisi kuna hizo parks!........
UNAFIKI WA VIONGOZI WA DINI NA UDHAIFU WA SERIKALI YETU
Miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la wanasiasa kutumika katika shughuli za kidini tena wakipewa hadhi kubwa utadhani wao ndio wasomi na manguli katika dini.
Hali hiyo imekuwa mbaya na kuhusisha viongozi wa kisiasa katika harambee za makanisani na misikitini kwa kuwatumia wanasisa.
Aghalabu ni rahisi kusikia mbunge, meya, waziri, katibu mkuu n.k. wakiongoza harambee za mamilioni kuchangia mambo kadha wa kadha katika dini zao.
Viongozi wa kisiasa ni wanadamu ambao kazi yao haimaanishi kuwaondoa katika mambo ya kiroho. Lakini hawa si viongozi wa dini na wala hawapaswi kupewa hadhi katika safu za viti vya mbele.
Wao ni waumini kama walivyo wengine na hiyo ndiyo haki yao.
Kwakutambua kuwa siasa ni mchezo mchafu viongozi hao wanatumia nafasi wanazopewa katika kufikia malengo yao ya kisiasa. Michango yao na jitihada zao si za kiuumini bali zimefungamanishw na matakwa ya kisiasa. Kwamba huko ndiko wanakotaka waungwe mkono kwa kutumia viongozi wa dini
Tunaelewa kuwa viongozi wa dini wana nguvu kubwa sana katika ushawishi wa waumini wao.
Mara zote wamekuwa wanasikilizwa hata kama hoja zao hazifikirishi. Si kiongozi kasema!!!!
Hivi karibuni kuna kiongozi maarufu amekuwa akipita makanisani na misikitini kuchangisha harambee.
Inasemwa kisias alicho changa hadi sasa ni mabilioni ya pesa.
Kiongozi huyo anyehusishwa sana na uchaguzi wa 2015 kupitia chama tawala amejitetea kuwa michango na pesa zake zinatokana na michango ya marafiki zake.
Utetezi huu dhaifu na wa kipuuzi unatupelekea kuamini kuwa kiongoz huyo eti amejivika wadhifa wa kufikisha michango ya waumini wenzake kwa mungu kama yeye na si kama wao.
Kwamba yeye amechukua jukumu la kidini la kuwafikishia michango hiyo.
Hali ni kama hiyo kama tunavyoshuhudia kila siku. Mara utasikia waziri wa imani fulani ameongoza harambee kanisani, mara meya fulani, mara katibu mkuu fulani n.k. Wote hawa hufanya hayo kama sehemu ya mtaji wa kisiasa.
Viongozi wa dini wanafahamu hali hiyo wazi na wanajua kuwa hilo litazaa balaa siku za baadaye na kupekekea uvunjifu wa utangamano wa taifa na imani kwa waumini.
Tumeshuhudia kukiwa na mijdala mikali hadi bungeni ambako wabunge wameasi vyama vyao ili kutetea imani na wala si wananchi waliowapeleka. Tumeona mivutano ya kidini ikiendelea na tumeona vurugu ambazo chanzo chake ni sababu za dini.
Viongozi hawa dini wanaowakaribisha wanasiasa kuwagawa wananchi wanafahamu madhara ya kile wanachokifanya. Wanafahamu kuwa mungu hapendezwi na unafiki wanaoufanya wa kuhubiri amani kwa mlango mmoja na kuchochea uvunjifu wa amani kwa upande mwingine.
Ikifika hapo nadhani wasomaji watakubaliana na duru za siasa kuwa viongozi hawa ni wanafiki kama kichwa cha habari kianvyosema.
SERIKALI DHAIFU
Katika siku za nyuma viongozi walikuwa waumini kama wengine huko misikitini au makanisani walikwenda kama waumini. Kama ilitokea kupewa hadhi basi ni kwa heshima ya nafasi zao na wala si kwasababu ya nyadhifa za kisiasa au ushawishi wa kutaka kuungwa mkono na viongozi wa dini.
Hata ilipotokea viongozi hao wakaombwa kushiriki katika mambo hayo mara zote wamekuwa wakiongelea mambo yanayolihusu taifa kama afya, umasikini elimu, umoja wa kitaifa, kutobaguana n.k
Siku hizi serikali imekaa pembeni kana kwamba imetoa ruhusua kwa mwenye dini au dhehebu fulani ni ruksa kutumia mwanya huo kujinufaisha kisiasa.
Ni serikali hiyo hiyo inayohubiri amani imekuwa mstari wa mbele kuachia hali ya uvunjifu wa amani kutamalaki.
Kuwaachia viongozi hao kutumia nafasi zao za kisiasa katika mambo ya kiimani ni jambo la hatari ambal serikali yoyote duniani haiwezi kufumbia macho.
Kiini macho ni pale matatizo yanapotokea, utasikia viongozi wakisema hata wao hawajui chanzo ni nini.
Tena wanasisitiza kutumia silaha za moto kukomesha wahalifu hao. Inashangaza kwasababu kwanini serikali itumie silaha za moto na si kuzia uhalaifu kabla haujatokea?
Kuachia hali za kuchangisha mabilioni huko miskitini na makasnisani ni kutengeneza mazingira ya uvunjifu wa manani na ni ujinga na upuuzi has kwa mtu mwenye dhamana kuamuru kutumika silaha kukomesha hali hiyo.
Huu ndio udhaifu mkubwa sana wa serikali ya JK katika miaka 50. Hatukuyaona haya siku za nyuma na serikali hii inalipeleka taifa mahali pabaya sana.
Serikali imeshindwa kuwakemea viongozi wake au wadini huku kwa unafiki ikisema haina dini.
Kama haina dini kwanini wanasiasa wanapita katika sehemu za dini kueneza siasa zao uchwara?
Duru za siasa zinawatahadharisha wananchi kuwa katika kutafuta muafaka wa kitaifa kwa mambo muhimu kama elimu, afya na umasikini kiongozi hupatikana kwa sifa na si imani.
Hawa wanaonunua uongozi kwa kutumia harambee wanawekeza na pindi wakipewa dhamana watautumia umasikini wa wananchi kurejesha fedha zao.
Ni vema kuwauliza kwani hawajengi shule na vituo vya afya eti ni hadi wapitie misikitini na makanisani?
Huu uumini wa siasa za makanisani na miskitini umeanza lini na una lengo gani.
Ni wakati umefika sasa kuwakemea viongozi wa dini kwa unafiki na kuikemea serikali kwa udhaifu.
Duru za siasa tunalaani hali hiyo kwa nguvu zote, tunawalaani viongozi wa dini na wansiasa wao kwa kutaka kulitumbukiza taifa katika janga kubwa
Tusemezane
Mgeni wa leo Kimweri
Oh! Kimweri! Shukran ndugu yangu kwa kugusa nafsi zetu.Nguruvi, Kuna mwerevu mmoja aliwahi sema maneno yafuatayo.namnukuu, "you can not solve problems using the same level of thinking,when you created them".
Wanachotufanyia viongozi wetu wa dini ni kutuaminisha kuwa kiongozi wakisiasa aliyeshindwa kutatua matatizo ya jamii wakati akiwa madarakani,ataweza kuyatatua kwa kuchangisha michango kupitia kwenye taasisi za dini.Mbaya zaidi haya yanafanyika katika hali isiyo na uwazi,na lugha za ujanja ujanja zikitumika.
Viongozi wetu wa dini nao,wameamua kutu-take for a ride.Halafu waumini wakiacha kuwafuata kwa weledi waliokuwa wanafanya hivyo zamani wanapanda juu ya membari na kulalamika maadili yanamong'onyoka.yataacha vipi kumong'onyoka wakati wewe kama kiongozi wa dini hauna "moral authority".
Leo hii makanisani na misikitini ndio kimbilio la wauza unga,kimbilio la wanasiasa wenye kashfa lukuki.
Imefika wakati sasa wazee wa makanisa na misikiti hawapewi heshima inayostahili na heshima hiyo wanapewa wenye nacho,kwa kuwa tu ndio wachangiaji wakuu wa hafla za makongamano ya kidini.
Suala lengine ambalo inabidi litazamwe kwa jicho la 3 ni uingiaji wa Taasisi za kidini kwenye shughuli za kibishara zilizopitiliza,sasa hivi hasahasa makanisa,ndio mabepari wakuu wa nchi hii,ndio wanamiliki mapande makubwa zaidi ya ardhi,ndio wamiliki wa shule nyingi za sekondari,ndio wamiliki wa vyuo vingi zaidi ambavyo si vya serikali,ndio wamiliki wakubwa wa kumbi za harusi pamoja na majengo kwenye miji yetu.Katika hali ya kawaida,complexity ya aina hii ya shughuli za taasisi za kidini inazifanya zifikirie kibiashara zaidi,kwani priority zao ziko kwenye kupata faida,kufanya investment na kutunza investment zao,kwa matiki hii tutegemee kuona mapadri na maaskofu wanao-act kama ma-CEO wa makampuni makubwa,kwani wana -vast interest za kutake care of.Dini ile tuliyozoea ya miaka nenda rudi inaelekea kupuuzwa,ukichanganya na uwepo wa serikali dhaifu isiyoweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo si jambo la ajabu viongozi wa dini waki-act kama wanasiasa/wafanyabiashara na watawala vilevile.,kwani serikali inayopaswa kuchora mstari juu ya mipaka ya viongozi wa dini iko bize kufanya harambee za kuchangia visima vya maji ambaavyo wao walishindwa kuvichimba.
hali tuliyokuwa nayo sasa kama taifa ni ushahidi ulio wazi kuliko wa aina yoyote wa "a failed state". nchi ya kusadikika haswaa
Ni mgeni wetu ambaye anaweza kutusaidia kwa undani nini mwenyekiti anafikiria.
Tunataka kusikia kutoka kila sehemu zina maoni gani.