Dunia Ya Wadhambi!!!!!!!

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,190
Natumai ni mabuheri wa afya!

Nikiwa O level nilitokea kupenda sanaa somo la literature haswaa ya west africa hususani Mzee Chinua Achebe na kazi zake za Things Fall Apart, No Longer at Easy, Arrows of God, na zinginezo! Pia kazi za West African writers wengine kama Cyprian Ekwensi na kazi zake kama White Ginesis, Beautiful Ones are not Yet Born, The Man of the People, Wole Soyinka pia kazi zake nimezisoma sanaaa.

Tukirudi literature/fasihi ya kwetu huku africa mashariki nayo nimeipitia sanaa hususani kazi za Ngugi wa Thiongo/ James Ngugi kama Wheep Not Child, I Will Mary When I Want, The River Between, na Petals of Blood. Pia kuna kina Okot P. Bitek na kazi zao za Song of Lawino and Acholi, kina Hayati Shaaban Robert, Hayati Mloka na kazi yake ya Diwani ya Mloka, Malenga Wapya, Prof Amandina Lihamba na tafsiri yake ya Hawala ya Fedha (Hii kazi kiuhalisia ni ya Cyprian Ekwensi wa Ghana)

Kutokana na mambo kadha wa kadha sikuweza kuendelea na Literature zaidi, ila katika vitu navopenda kujifanyia maishani kimoja ni kujiendeleza kwenye hii Literature. Saa hivi najiendeleza online katika haya mambo ya kuwa Author, na katika part ya term paper natakiwa kuwasilisha kazi yangu binafsi ya Kiliterature! Kazi inatakiwa kuwa Kingereza ila kwa mapenzi yangu binafsi original work naifanya Kiswahili then nitaipeleka Nairobi ikatafsiriwe professionally in English ili kujipatia Maksi zaidi!

Kwa kurecognize kuwa times zimechange mandhari ya hii kazi yangu ya Dunia ya Wadhambi itakuwa inaongelea mazingira ya leo ya Tanzania Urban na Kijijini!. Tuwe Pamoja!

CHAPTER 1

(2005) Aikaeli!

Nimekaa naafakari miaka yangu hii 40, mimi Aikaeli sina mume wala mtoto, niko peke yangu mkiwa huku duniani. Kwanini nimekuwa katika hali hii? Wenzangu wote wana watoto wakubwa na waume zao, wametulia kwenye ndoa zao. Japo kuna wachache wameachika baada ya ndoa kuwashinda ila angalau walijaribu! Uzee wanijia kasi sana! Siku za ujana wangu na siku za furaha yangu zimeisha kama utani.

Sio kwamba sikubahatika mtu wa kunioa, la hasha watu wengi sanaa, vijana na wazee walipenda sana tuishi maisha yetu wote japo mimi kwa wakati huo sikuona umuhimu wa kufanya hilo. Mungu alikuwa mwema sanaaa kwangu, na mpaka mda huu bado ni mwema pia. Kama ni uzuri mimi ni mzuri sanaa, japo unaanza kupotea na makunyanzi kujongea. Ila ningali binti mdogo sanaa watu waliniponza kwa kunisisitiza mimi ni mzuri kupita wengine na nikajenga kiburi juu ya hilo.

Sikujua tu kuwa uzuri ni wa kupita, na iko siku kama leo nitabaki nashangaaa umepitaje! Nimetoa mimba zaidi ya 5 na usinihukumu kwanza hadi ujue nini kilinisibu hadi nikatoa mimba zote hizo.
Nimewahi kuishi na wanaume 6 tofauti ila hakuna hata mmoja niliedumu nae na kumuita mume au mwanaume wa maisha yangu. Wote tulishindwana na kila mtu akachukua njia yake! Usinihukumu kwanza hadi ujue nini kilinishinda kwa wanaume hao!

Nakiri dunia hii ni ya wadhambi, na mimi ni mdhambi mmoja wapo! Nimefanya dhambi nyingi sanaaa mpaka kuna wakati najiuliza "Je ni kweli kuwa Mungu anasamehe dhambi zote hata zile mbaya kuliko?" Napatwa na mashaka japo naiamini biblia! Binafsi nimetendewa dhambi nyingi sanaaaa, na mie nimewatendea watu dhambi nyingi sanaa pia! Nikifikira kama kweli Mungu yupo na Jehanamu ni ukweli ipo na sio story nahisi nitafanywa kuni huko.

Na hii ndo simulizi ya Dhambi zangu ndani ya dunia yetu hii ya wadhambi! Eee bwana Unihurumie!

(2005) Claire

Kwa haraka haraka umri wangu ni kati ya miaka arobaini, japo watu wakiniuliza nasema 30, 35, 36 wowote utakaonijia kichwani! Mi naamini umri ni namba tu wala sio jambo la kutilia mkazo! Claire mimi mtoto wa kariakooo, mwana wa Mwanahamisi, mjukuu wa Chiku kwa hakika jiji nalijua! Nalijua jiji na mataa yake.

Sijafanikiwa sanaa kimaisha japo nina mtoto mmoja Abul Latiff au John maana nilisikia baba yake alimbatizaga, ambae sijui alipo wala anafanya nini, ila ukinilinganisha na mama yangu Mwanahamisi Mwinyimvua na Hayati bibi yangu Chiku bin Saidi nimejitahidi sanaaa! Nina nyumba nimeijenga mwenyewe (kiufasaha nilijengewa na bwana wangu wa Kitwana mnyamwezi wa Tabora huyo, mfanya biashara wa Tumbaku) Sinza huko, nimeipangisha mie bado naishi Kariakoo hadi na leo! Hata kesho Inshaaalah nitakuwepo Kariakoo.

Claire ni jina tu nilijipa mwenyewe katika harakati zangu za kusaka maisha kuendana na wakati! Jina langu halisi lilikuwa Sultana bin Seif Abdul Basit, na asili yetu ni waarabu wa Muscut tuliochanganyika na watwana wa kimanyema na wangazija kidogo! Wengi hutuita mashombe shombe au waarabu koko.

Nililelewa katika hali ya Uislamu safii na kuswali swala tano, Nimesoma Madrasa sanaa nakuweza kuwa Sheha, na hayati baba yangu alikuwa tayari kunipeleka hija na mimi nije kuwa Hajat siku moja. Kwa kweli nilipo leo siwezi mlaumu mzazi wangu kwa lolote.

Japo kitabu nasoma mara moja moja kwa taabu sanaa, na kuomba dua za hapa na pale ila simo miongoni mwa wasafi wa dunia hii hata chembe. Pombe nanywa sanaa tu na nguruwe pia nala wenyewe makafiri wanaita pork au kitimoto. Mola anipunguzie ghadhabu yake na kunijalia hisani ya toba ya kweli kabla maut haijanikuta.

Ilikuwaje hadi nikajikuta hapa nilipo ni habari ndefu kidogo ila mda ninao wa kuwaelezeeni.

(2005) Alexa

Hapa nilipo siamini kama kuna Mungu wala sijawahi kuamini kama kuna Mungu yupo tangu niwe na akili zangu timamu. Nilipokuwa mdogo sanaa nakumbuka mama alikuwa ananipeleka sunday school na dunia ilijaa matumaini. Lakini baadae ndo nilipofikia muafaka kuwa hakuna Mungu na kama yupo ni kwa maslahi ya watu wachache tu.

Japo siamini katika Mungu ila naamini katika kuwatendea wengine wema. Japo hili kwangu limekuwa gumu sanaaa, na lisilotekelezeka. Labda imekuwa hivi kwa sababu ya maovu niliyotendewa mie na walimwengu au kwasababu ukiwa mdhambi dhambi itakufuata tuu! Sijawahi fika muafaka na kujua sababu haswaa ni ipi.

Nimetenda mengi ambayo hayaipendezi jamii na mengine naendelea kutenda hadi sasa. Miaka yangu yote 38 nimekuwa na matumain kuwa Mungu atanipata tu huko niendako na bado sijakata tamaa kabisaa ila matumaini yanafifia kadri miaka inavyosonga. Uzuri ni kuwa sijawahi lipia mabaya niliyoyatenda mpaka mda mwengine nawaza kuwa huenda Mungu nanifidia ule ubaya niliotendewa.

Pamoja na yote nashukuru kuwa nimeweza kutekeleza agizo alilonipa Mama la kumlea Alex mdogo wangu kwa ghara yoyote ile, japo haikuwa rahisi ila nimejitahidi. Vinginevyo maisha yangu yamekuwa ya kawaida na kukosa mvuto kabisaa. Japo nimetokea ukoo tajiri sanaa na baba yangu bado ni tajiri na anaishi kifalme ila sisi tunahangaika, na tutaendelea kuhangaika.

Ndoto yangu kubwa ni kumuona Alex anaishi maisha mazuri ya kumpendeza Mungu na jamii! Japo kanisani mimi binafsi sijakanyaga sijui tangu lini ila Alex lazima aende, na amepata sakrament zote, na nasimamia aendelee kuhudhuria.

Ninaishi sababu naishi tu, na nimeshi hivi mda mrefu sanaa, na nitaendelea kuishi hivi hadi hapo nitakapopata sababu ya kuishi kivingine.


ITAENDELEA!!!!!!!!!!
 
Sio kwamba nakukosoa
but ungetumia style ya wewe kusimulia
kuliko ya huyo Aikaeli kusimulia..
ingependeza zaidi....
 
Sio kwamba nakukosoa
but ungetumia style ya wewe kusimulia
kuliko ya huyo Aikaeli kusimulia..
ingependeza zaidi....

Hahahaaaaa! The Boss mkuu nashukuru kwa ushauri wako ila hii term paper ni complex sanaaaa, manake inabidi utumie form zote za usimuliaji ikiwemo narration ambayo unaisema wewe, Dialogue ambapo kutakuwa na majibizano, na expression ambapo character anajielezea mwenyewe kama hapo nilivoanza!

Pia haitakiwi hadhira ijue muelekeo, mtririko na mwisho story itaishaje! Yaani msomaji asiweze kupredict next kitafuata nini, na mwisho itakuwaje! Hii ni neo/liberal literature kama za kina Sydney Sheldon, Robert Laudm, Daniel Steel, na Jackie Collins. Kuna guidelines/muongozo na adhere to hapa ndo unaoleta UTRATRA!
 

OK ngoja tuone itakavyokua but hii style itaku limit
hutaweza kutoa habari za characters wengine in deep
since msimuliaji ni one of the character pia..
 
Mimi si mtaalamu sana wafasihi ila nimesoma hapo juu nimevutiwa japo kuna makosa madogo ambayo yawezekana mimi nimeyaona ni makosa kumbe ni vionjo..........mfano hapo uliposema mie nafikiri lingetumika neno mimi pia uliposema story nafikiri hadithi lingefaa zaidi ili kuleta msisimko wa matumizi halisi ya lugha ya kiswahili

Huu ni mtazamo wangu binafsi kwa namna nilivyopitia hii simulizi lakini kwakuwa umesema itatafsiriwa basi haina shida sana

Best wishes..
 
congrats gal....hata mie nimekuwa mpenzi wa literature since o-level, navutiwa zaidi na kusoma literature coz imenihelp sana kwenye kujifunza lugha zingine, its nice....hope utafika mbali na dream yako......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…