Dunia Ya Waarabu I-Karibu Nasi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia Ya Waarabu I-Karibu Nasi!

Discussion in 'International Forum' started by maggid, Jan 30, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  MOTO unazidi kuwaka Cairo, unasambaa pia. Tumeona picha za askari wale vijana wakitabasamu na kupeana mikono na wananchi. Ni ukweli, wengi wa wanajeshi hao wamekuwa recruited ( kuingizwa jeshini) wakitokea kwenye familia za kimasikini.
  Kwa wanajeshi hawa, wana uelewa mkubwa wa wanachokipigania watu wa Misri. Ni suala la wakati tu kabla wanajeshi kuchukua uamuzi wa jumla wa kusimama upande wa umma. Na hilo likitokea, basi, mwisho wa zama za Hosni Mubarak utakuwa umeharakishwa, kwa nguvu ya umma ukisaidiwa na jeshi.


  Maana, hata Hosni Mubarak akifanikiwa kuning’inia madarakani, bado, siku zake zitakuwa zikihesabika. Hosni Mubarak hana support ya umma, hivyo basi, hana uhalali wa kuendelea kuongoza dola kubwa na kongwe ya Egypt.


  Watawala Afrika wana cha kujifunza?
  Katika Afrika, mtawala atakayepuuzia moto unaowaka katika Dunia ya Waarabu ama ni mgonjwa au ni mjinga tu . Ni ukweli, kuwa Dunia ya Waarabu i-karibu nasi sana. Ni mwendo wa saa tano tu kwa ndege kutoka Dar es Salaam, Nairobi au Kampala kabla ya kutua Egypt, Tunisia, Yemen au Algeria. Ndio, ni umbali mfupi sana kabla ya aliye kwenye ndege kuanza kuuona moshi wa moto unaotokana na moto uliowashwa na umma unaotaka mabadiliko.


  Ni dhahiri, kuwa yanayotokea kwenye Dunia ya Waarabu yana athari kubwa kwa ‘ Dunia Ya Waafrika’. Kihistoria na Kiutamaduni, Waafrika tuna mengi yanayotufanya tuwe karibu na Waarabu. Yaliyokuwa yakitokea Ulaya Mashariki miaka ile ya 80, ingawa yalisaidia kuleta mabadiliko pia barani Afrika, lakini, bado, yalitokea mbali na Afrika.


  Lakini, harakati za vijana wa Kiarabu kuleta mabadiliko na hata kufanikiwa katika harakati zao, yana kila uwezekano wa kuwatia hamasa vijana wa Kiafrika katika nchi zao. Ikumbukwe, mengi wanayopigania vijana wa Kiarabu yanafanana na ya wenzao wa Afrika.  Inahusu ukandamizaji, mgawanyo wa rasilimali wa haki na kukua kwa demokrasia ili kuchangie ustawi wa mataifa yao. Kupelekee kupata ajira na kuongeza vipato vyao. Kwa vijana hawa, kukua kwa uchumi wa nchi zao hakuna maana kama hali za watu wa kawaida zinakuwa ngumu kila kukicha na huku pengo la walio na wasio nacho likikua kwa kasi ya kutisha.
  Kwa viongozi Afrika busara ni mapema kupunguza nywele zao kabla ya kulazimishwa kutia maji na kunyolewa vipara! Inahusu mabadiliko makubwa ya Katiba za nchi zetu ambazo bado zina ukakasi wa enzi za ‘ Chama Kushika Hatamu Zote’. Dunia Imebadilika.
  Maggid
  Iringa,
  Jumapili, Januari 30, 2011
  mjengwa
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa ndugu yangu! lakini tatizo kubwa ambalo limejaa kwenye vichwa vya viongozi wa kiafrika ni kwamba hujifunza tu yale ya kuwanufaisha wao! Unakumbuka maneno ya Gadafi wakati Ben-ali alipokimbia! Anasema eti wananchi wa tunisia walikosea na bado yeye akaona kwamba mfumo wake wa utawala ni mzuri. Ingekuwa ni mbinu mpya ya kuiba kura wangeiga haraka sana, lakini kwa sababu kinachotokea ni kunyangánywa utawala hawataki kabisa kurekebisha kasoro ila ni kuimarisha ubabe.
   
Loading...