Dunia ya sasa ni ushindani si lele mama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia ya sasa ni ushindani si lele mama

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Nguruvi3, Jul 31, 2012.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanajamvi,
  Awali ya yote niwatake radhi nitakao wakwaza kutokana na kauli zangu.
  Sina lengo baya zaidi ya lile la kuboresha.

  Ukitembelea majukwa mengi hapa JF, japo basi unaweza kutoka na kitu. Niseme wazi jukwa la elimu ambalo nilidhani lingeng'ara kwahakika limedoda.

  Jukwa limegeuzwa sehemu ya kusemana na kutafuta CV za watu,kuomba past papers, aidha limekuwa la kupeana taarifa za mikopo badala ya maarifa ya kieleimu.
  Hayo hayana ubaya lakini yasiwe ndio sehemu kuu ya jukwaa la elimu.
  Jukwaa lazima libebe maana halisi ya elimu na si kwasababu tu!

  Katika dunia ya sasa elimu siyo diploma,degree za uzamili au uzamivu. Elimu ni namna gani utaweza kukabiliana na mazingira magumu ya ushindani. Kwa sasa tumeanza na soko la pamoja la EAC lakini pia sisi tukiwa kama sehemu ya dunia tunachanganyika na watu wa mataifa mengine. Kuna fursa nyingi tu zinazoweza kubadilisha maisha yetu.

  Mathalani, nimesoma mara nyingi watu wakiuliza kozi gani bomba au inalipa. Ukweli wa mambo ni kuwa kila kilichopo duniani ukiweza kukitumia vizuri na kwa maarifa kinalipa. Lakini pia lazima uelewe kuwa milango haipo wazi kana kwamba utaweza kupata kila kitu kama unavyotaraji.

  Kozi kama za ualimu watu wengi wanaziona kama hafifu lakini hawajui kuwa ndizo kozi zenye milango mingi sana na zinazoingiliana na kozi nyingine kwa namna moja au nyingine. Nitumie msemo wa mitaani kozi ya ualimu ni kama 'funguo malaya' inayoweza kufungua kila mlango. Tatizo watu hawaangalii mambo kwa mtazamo mpana na hapo kuna kupotea kwa hali ya juu.

  Ni lazima ujiulize pia endapo kozi 'bomba' unayoitaka katika maisha yako itaweza kukupa fursa!!.
  Dunia imebadilika, kuna wasomi wengi wenye sifa wanazurura, sasa mwenzangu uliyehitimu juzi tu kama unadhani umefika ukweli ni kuwa hujafika.

  Soko la ajira la sasa haliangalii Degree yako au GPA, linaangalia wewe kama mwajiriwa utaweka nini mezani kulisaidia shirika ua taasisi. Una ujuzi gani zaidi ya degree yako ambayo kila mtu anayo na wengine wanazo kutoka katika vyuo vyenye heshima.

  Ikifika hapo kuna mambo yanajitokeza:

  1. Una kitu gani kinachokutofautisha na washindani wako wengine? Nafasi moja ya kazi inaweza kuwa na candidates 300, sasa kwanini wewe uajiriwe na si Mr au Miss X ambaye licha ya ukubwa wa degree yake lakini pia anauzoefu kukuzidi. Wenye lugha zao wanasema 'how do you stand out of the crowd'.

  2. Unawezaje kujiuza kwasababu nyote mliopeleka CV mnabidhaa ile ile, sasa kwanini waajairi wadhani bidhaa zako ni bora zaidi ya zile 299 zilizojitangaza kuwania nafasi hiyo.

  Hapa kunaingia vitu vingine kama ifuatavyo:

  a)Ni kwa vipi CV yako imeweza kupenya na kuwa short listed katika zile 10, kutoka zile 299 kwa ajili ya Interview.
  Kumbuka usipokuwa short listed basi huna interview na huna kazi hata kama una degree zako na GPA safi.
  Kwahiyo unatengenezaje CV (Resume) yako ili ukubalike katika kuingia katika 10 bora ni muhimu sana.

  b) Katika 10 bora watakaoitwa katika interview utawezaje kuwashawishi jopo la watahini ili uwe ndani ya 3 bora?
  Hapa ndipo mbinu za interview zinapokuja.

  Hapa nimejaribu kutoa tu muhtasari wa namna gani dunia inakuwa ya ushindani hata kama una nondo zote.
  Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, kuwa na Bachelor, master au PhD bado hakujakuhakikishia makali katika ushindani wa dunia ya leo. Ni jinsi gani unajiuza na unaweza kuuza hizo degree zako ni muhimu sana.

  Tena teknolojia imesonga mbele hizo CV zinachaguliwa kwa computer, sasa hapo suala la kujuana 'technical know who' halipo. Matokeo ya yote utaishia kukimbilia ukabila na udini wakati ukweli ni kuwa hujui kujiuza au kuuza bidhaa zako.

  Hebu tuangalie mambo yaliyosemwa hapo juu, kozi, kuandika CV, kufanya Interview n.k
  Wenye jukwaa kama mtaridhia basi tutaendelea kudadavua kwa kiasi tunachoweza ili kupeana maarifa.

  Noamba kutoa hoja.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hoja nzuri na wakati sahihi. Badala ya vijana kutumia muda mwingi kutafuta wa kumlaumu, ingefaa watumie muda huo kwenye jukwaa la elimu na kubadilishana maarifa.
   
 3. Aqua

  Aqua JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 23, 2012
  Messages: 1,299
  Likes Received: 418
  Trophy Points: 180
  Hoja nzuri,maelezo mazuri.Majukwaa mengi siyo la elimu tu yamekuwa yanatumika ndivyo sivyo,sijui mtu anazani akijisajiri JF anakuwa great thinker automatikali.Kuna mtu anaandika kitu unashindwa kumwelewa.So nasupport mchango wako,ukicheki folamu za wenzetu watu wanaomba msaada kwa mambo ya muhimi,na watu wanasaidiana kiukweli.
  Back to your point,ajira sasa hivi competetion nikubwa watu wanazani kuwa na degree ndiyo kila kitu.Kuna "skills" zinahitajika kama
  Interpersonal skill
  Leadership skills
  Computer skills
  Language skills
  Negotiation skills,etc
  wengi hatuzijui hizi,na wengine huziandika kwenye cv zao bila kuzijua ni nini hasa.Skill hizi zingine hatufundishwi mashuleni,ni wewe mwenyewe kwa bidii zako.Ni hayo tu
   
 4. S

  Slaker JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bonge moja la idea mzeiyah,ime reach a point 2funguke vjana wa ktz 2cje achwa na hili basi la asubuhi..... ...big up.
   
 5. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  nadhan leo umenipa kitu cha maana sana...aise nashkuru sana..na hii ndo iwe maana JF! mi binafsi nimekukubal kwa hil wazo olako!! big up saaaaaaaana!!
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Inaendelea ktukoa mwanzoni......

  Kozi: Tumesema kuwa wapo watu wanaodhani ukifanikiwa kupata kozi fulani basi mambo yatanyooka. Hili linatokea kuanzia huko sekondari hadi vyuoni. Watu hawangalii uwezo wao na kile wanachokiataka kukifanya. Aghalabu utasikia nataka niwe Daktari, lawyer au Engineer pengine kwa kudhani kuwa uwepo wao huko ni alama ya heshima na uwezo

  Ukweli ni kuwa unapofanya kile unachokipenda na si kile unachopendezwa nacho basi uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa sana. Katika dunia ya leo kinachokusaidia ni jinsi gani unaweza kutumia fursa ili kujiendeleza na si masomo gani unayosoma. Mfano mzuri ni ule wa kudhani kozi za Art ni hafifu kuliko za Science. Ukitazama kwa undani watu waliofanikiwa ni hao wanaonekana dhaifu na si wale waliong'angana ilimradi tu nao wawemo katika kundi.

  Kuna kijana mmoja alianza na kozi ya diploma ya ualaimu, halafu akajiunga na chuo kikuu katika kozi ya B. Science general. Baada ya hapo akajiunga na kozi za utafiti wa wanyama. Kwasasa hivi ni mmoja kati ya wanasayansi wakubwa duniani na hakika maisha yake yamebadilika sana. Huyu alianza kama Mwalimu na sasa ni mtafiti wa kutumainiwa tena katika mataifa makubwa.

  Nimesoma maoni ya watu katika nyuzi mbali mbali zikisema mwisho wa Engineering ni degree ya kwanza kwasababu master au Phd hazina mashiko. Lakini jiulize kama mtu amesoma engineer na kisha kupata kozi nyingine kama MBA unadhani soko lake lipoje. Focus ya mtu isiwe engineer bali engineering itamwezeshaje yeye kubadili maisha yake katika sekta yeyote ile.

  Katika nchi yenye upungufu wa watalaam kama Tanzania, mwalimu anaweza kubadili taaluma yake na kuwa mwandishi wa habari. Tunakoelekea ni kule ambapo mtu anakuwa na taaluma za kutosha zimwezeshe yeye kusonga mbele.
  Mathalani, mwandishi wa habari za afya ambaye ni Daktari anasoko zuri kuliko mwandishi tu wa habari.

  Mwandishi wa habari anayejua mambo mengi ya kijamii anafursa nzuri tu kuliko mwandishi wa habari anayesubiri kuandika kilichosemwa.

  Lakini pia kama umesoma Bsc general au Ba. general kwanini usifikiriekuwa kuna nafasi unazoweza kuzipata kwa kutumia fursahiyo? Unapokuwa na kitu general ni jambo jema lakini ni vizuri zaidi ukawa na speciality. Speciality inakupa nafasi zaidi miongoni mwa watu wengi. Bsc yako unaweza kuielekeza katika Biology na huko ukazama katika vitu kama zoology, wildlife, environment control n.k.

  Ni muhimu ukaelewa kuwa kozi peke yake haijaweza kukupa ufumbuzi wa suala la ushindani. Ushindani ni jambo jema lakini kama una nafasi ya kupunguza huo ushindani basi fanya hivyo. Nina maana kuwa ukisoma kitu jaribu kuwa na vitu vya ziada. Huwezi kuwa archtect mzuri kama hujui kutumia computer na program zake zinazohusu fani yako vizuri.

  Huwezi kuwa mwandishi mzuri kama hujui njia za kuapata habari za dunia kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano iliyopo duniani kwa sasa. Huwezi kuwa Daktari aliyefanikiwa kama hujui mbinu za utawala na usimamizi wa vitu kama miradi.

  Hoja yangu hapa ni kuwa uzuri wa fani unaoutaka hautoshi ni lazima uwe na vitu vya ziada ili uwe 'total package'
  Kuna vitu vingine huwezi kufikiria ni muhimu lakini dunia ya leo ni muhimu sana.

  Nikupe mfano wa kuchekesha, endapo itatangazwa kazi na katika watahiniwa 299 umefanikiwa kuwemo katika 3 bora, hapo maana yake ni kuwa nyote watatu mnavigezo amabavyo mwajiri wenu anavitaka 'potential candidate'
  Suala linakuja ni nani ambaye ni bora kuliko wenzake.

  Mchanganuo wa kazi ni wa utafiti 'research' ambayo mtahiniwa anatakiwa asafiri kila mara ima kusimamia, kuongoza au kukusanya takwimu. Mwajiri ataangalia vigezo vyote na kuona mmefungana.

  Hapo mwajiri atatoka nje ya vigezo vya kazi (CV/Resume) na kuangalia vitu vingine. Katika watahiniwa wote watatu, wakwanza ana GPA kubwa tu, wapili ni mzuri wa takwimu na watatu hafikii vigezo hivyo lakini anakitu kimoja, nacho ni leseni ya kuendesha gari.

  Usijeshangaa huyu mwenye leseni akapata ajira kwasababu yeye kama wengine anauwezo wa kufanya kazi tarajiwa, lakini atalisidia shirika au taasisi kuondokana na bajeti ya kuajiri dereva.

  Huyu inaweza kuonekana amependelewa lakini ukweli unabaki kuwa yeye ni msaada na si mtegemezi. Vipi kama hao wawili wa mwanzo wangekuwa na leseni hata kama hawana gari!!
  Inachekesha na kuonekana kama ni ujinga, trust me, dunia ya leo mwajiri anataka assert na siyo liability.

  Hapa nina maana kuwa degree yako ikusaidie kufikia malengo mengine, wenyewe wanasema 'diversify' ya kwamba wewe ni Engineer, lakini pia unauwezo na ufahamu mzuri wa computer na una certificate ya project management. Zaidi ya hapo umefanya MBA yako kwahiyo una skills zote za management.

  Lakini pia jiulize, je una vigezo vya mwajiri anavyovitaka kama lugha? ni kwanini basi baada ya kupata degree yako usifikirie kunyoosha lugha yako kwa kozi ndogo ndogo, mathalani kule British council. Hutuwezi kuepuka suala la lugha vingnevyo tutabaki tukilalama, wakenya wanaajiriwa, warundi wanaajiriwa! ni lazima tuwe 'fit' kwa ushindani

  Hayo tu hayajawa silaha nzito za kupambana na ushindani, bado una kazi ya kumshawishi mwajiri kuwa una haki ya kupata mwaliko wa interview. Ushawishi huo unatokana na jinsi gani umeandika taaluma yako na kumvutia mwajiri na je kweli ni wewe umeandika? hapo yanakuja masuala mawili
  1.CV/resume writing
  2. How do you present your CV before the panel

  Itaendelea.......
   
 7. B

  BARAKA FESTUS Member

  #7
  Oct 21, 2014
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa kaka,
   
 8. k

  kombo mzalendo Senior Member

  #8
  Oct 21, 2014
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uko vizuri mkuu endelea kutuelimisha mkuu
   
 9. kijimsela

  kijimsela Member

  #9
  Oct 21, 2014
  Joined: Mar 17, 2013
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kweli kabisa mkuu
   
 10. keynessian

  keynessian JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2014
  Joined: Feb 28, 2014
  Messages: 479
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Hongera mleta mada kwa elimu uliyoleta , naomba kueka mawazo tofauti kidogo, Naona content ya maelezo yako imegusia sana kujiandaa kwa ajili ya kuajiriwa kiukweli competence unayoongelea siyo mwarobaini wa tatizo la ajira kiuhalisia , pia haimaanishi kwamba ambao hawana izo comptencies ndo waliokosa ajira, kuna watu wana vigezo vingi na elimu kubwa na bado hawana ajira, ushawahi kufikiri itakuaje kama kila mtu akiwa competent kama unavyosema itakuaje? Je ajira zitaongezeka? Obviously jibu ni hapana ukweli ni kwamba nafasi za ajira ni chache kuliko wanaihitaji kwa iyo tatizo litabaki pale, Nataka kumaanisha nini? Lazima tufikirie kwa mapana namna ya kutengeneza ajira nikiimanisha kujiajiri, iyo competency unayoongelea tujitahid kutumia kutafuta fursa za kujiajiri na kuzifanya katika hali yenye tija Jambo ambalo litaweza kutengeneza ajira zingine pia!
   
 11. Ighombe

  Ighombe JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2014
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 892
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 60
  Nimeimenda in this way jukwaa linakuwa hai.
   
Loading...