tilmikha
JF-Expert Member
- Feb 27, 2013
- 496
- 605
Habari zenu wapendwa!
Nimekaa na kutafakari mno kwanini wazee wetu waliifananisha dunia na tambara bovu ilhali kila mmoja wetu anapigana usiku na mchana kuhakikisha anapata chochote kile kitu kitakachomuwezesha kuendana na hali ya hii dunia iliyofananishwa na tambara bovu. Wapo wanaofariki kwa kupigania maisha na wapo wanaoonekwana wamewin katika maisha lakini kwanini waliifananisha dunia na tambara bovu licha ya kujaa anasa na starehe zilizojaa ladha tofauti tofauti!! Labda kwakua watu hufa na kuiacha dunia , au labda pengine aliebuka na msemo huu alikua ashajikatia tamaa ya maisha , yalimfika ya kumfika ndio badae akaja na huu msemo wa dunia tambara bovu.
Ila for somehow nahisi walikua sahihi na naamini hata na wewe ukimaliza kusoma huu uzi sote pamoja tutaungana na hawa wazee kuamini kuwa dunia ni tambara bovu.
Hakuna yoyote yule ambae ameifahamu dunia na hali za watu wake pamoja na fitina zilizojaa na starehe za mda mfupi ila lazma atakua amewafahamu hawa wazee walikusudia nini?
Na mtazamo huu daima huwa mtazamo wa mtu mwerevu na mwenye akili iliokomaa, anaeona pale wengine hawawezi kuona, katu humkuti kukata tamaa kwa kushindwa kuyafikia malengo yake, au kupaparika roho na kukodoa macho kwa yale aliyoyakosa.
Anafahamu kuwa kila furaha na ustawi mzuri wa maisha ya mtu afya aliyonayo hapana budi kuna siku vyote vitapotea, ama kumalizka. Basi kwanini ufike hatua ukate tamaa, uwaze kumaliza uhai wako ,kwanini uthubutu kuua mtu just kwa kitu kidogo tu!!!
Wazee walioposema dunia tambara bovu hawakukusudia dunia kama yenyewe kuwa ni kitu duni au haina maana at all, bali yale matendo yafanywao na walimwengu kila siku ndio inaifanya dunia iwe kitu duni . Usaliti, mauaji , dhulma , chuki.... haya yote yanaifanya dunia iwe tambara bovu.
Dunia ni mahala pa huzuni, upweke , na msongo wa mawazo uliopitiliza na mambo haya hakuna budi kila mtu lazima atakua nayo i.e stress, anxiety and depression.
Ubaya zaidi wa hii dunia ni kwamba once itakapo kupa furaha kidogo basi itakuliza sana, na ikikufurahisha sana itakuhuzunisha sana, naam huo ndio ukweli, hakuna nyumba yoyote ile ilio na furaha ila ndani yake itakua na sehemu ya huzuni, si nyumba ya raisi , si nyumba ya malkia wala taajiri yoyote yule ambae unaamfahamu wewe. Naamini hata kwako kupo hivo hivo naam hii ndio dunia .
Mara ngapi tumepokea ghafla habari za vifo vya mabilionea, pamoja na watu maarufu au wenye uluwa serikalini? Si ni juzi tu tulimzika mzee wetu Mengi, ushamsahau Steve Job? ndio dunia ilivyo vyovyote mtu itakapomneemesha basi lazima ama atakufa aache kila kitu ama atafiliska awe Bancrupt!!!
Diama dawama furaha hufuatiwa na huzuni, kicheko hufuatiwa na kilio na mda mwengine maumivu na mateso yasio na kifani , hivi hukuwahi kuyapitia haya!? Ila uzuri always yanakua ni yakupita tu. Nina mengi ya kuyaandika ila kwa sasa wacha nikuache na wewe utafakari halafu nitaendelea kukuonesha wazee kwanini waliifananisha dunia na tambara bovu ila sitohishia hapo bali kufahamishana namna nzuri ya kulitumia hili tambara bovu.