Dunia sio Salama

Dunia sio Salama

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,615
Reaction score
929
Wote tunajua kwamba ndege ya Malaysia imepotea takrabani wiki mbili sasa na wala haijulikani mahali ilipo. Kuna juhudi mbalimbali za mataifa ya magharibi na mashariki yanaangaika kuitafuta lakini bila mafanikio. Kwa sasa mimi kama mwananchi wa dunia ya tatu au nchi zinazoendelea nimejiuliza maswali mengi sana;

  • 1. Kama nchi zilizoendelea zimeshindwa kuipata hiyo ndege duniani kuna usalama gani? Hapa ina maana kwamba nchi zilizoendelea zimejiimarisha zaidi kiteknolojia, wameweka rada na setelaiti kila mahali hasa kwenye anga za juu ili waone kila kitu kinachoendelea duniani.
  • 2. Sasa dunia tujue lipi? Abiria wapo hai au wamekufa? Kama wamekufa maiti zao ziko wapi?
  • 3. Malaysia ni nchi ambayo imepiga hatua sana katika maendeleo ijapokuwa kwenye miaka ya 1960 ilikuwa karibu sawa na Tanzania, hata matokeo makubwa sasa (the big results now) Tanzania iliiga kwao, sasa na wao walifanya juhudi gani kuhakikisha usalama wa abiria na mali zake? Kwani hawakujua hujuma zilizokuwepo kabla (if any)? Au wanategemea mataifa ya magharibi yaangalie usalama wao?
  • 4. Nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania tumejifunza nini kutokana na mkasi huu? Kuna haja ya kuendelea kuzitegemea tena nchi za magharibi kwenye maswala yetu mbalimbali ikiwamo maswala ya ulizi na usalama?
  • 5. Je Tanzania ni salama kwa Utegemezi wa Marekani?
Naomba sana Moods msiondoe Uzi huu au kuuhamisha, uzi huu kwa mtazamo mfupi inaweza isionekana ya kisiasa lakini ukweli ni kwamba ni siasa tupu. Nchi zilizoendelea zinatumia technolojia zao kututisha na hata kutulazimisha tufuate siasa wanazo zitaka, wote tunajua yaliyomkuta Ghadafi , Sadam na wengineo. Hapa sio kwamba ninabeza technolojia ya nchi za magharibi bali tafakari pana kama technolojia zao zinaweza kukabiliana na changamoto za sasa. Yaani kwa mshangao wangu ni kuwa wao wana masetilite kila mahali mpaka kwenye mwezi wameshindwaje kuiona hii ndge ilipoelekea? Technolojia zao ni chui la makaratasi? Yaani technolojia zao zilitufanya tufikirie kwamba hata tukilala usiku na wake zetu hawa wajamaa huwa wanatuona. Naomba kuwasilisha
 
dah kazi kweli na hawakubali kabisa kusema imetekwa.....kuna nini hapa? Binafsi hata mimi nimeshindwa kuamini hali hiyo ya kuangukia baharini halafu resources zote zimetumika na bado bila bila?
kama imetekwa ni wazi kwamba aliyefanya hilo tukio ana technolojia kubwa kuliko ya hawa tunowaamini kwamba wako mbele kiteknolojia!
 
ndege haijatekwa itakuwa imepotelea kwenye sayari nyingine za mbaliiiiiii huko...wafanye mpango kwenda kuitafuta na huko
 
just imagine, kam ni ugaidi tumekwisha
 
ndege haijatekwa itakuwa imepotelea kwenye sayari nyingine za mbaliiiiiii huko...wafanye mpango kwenda kuitafuta na huko
sasa Mmarekani si anajifanya yeye ni mtaalamu wa sayari za juu, basi atuambie ndege iko wapi...au ni yeye ameiteka halafu anatuzuga?
 
ukiona hivyo ujue sasa kumbe aaaaaah MUNGU yupo. maana hapo ndipo MWENYEZI MUNGU anapowakumbusha wanadamu mipaka yao na uwepo wake.
 
siku.zote hao mnaowaita MAGAIDI wana akili kuliko hao wamarekani mnao waabudia

Na bado huu ni mwanzo tu
 
This is Paranormal phenomena, kuna uwezekano kuwa ndege hii haijaanguka wala haijatekwa, abiria wote wako hai somewhere
 
ndo mana tunaambiwa to live it to the fullest ,with love and doing what u want ,mana anything can happen at any time...kila nikiwaza daaah,naogopa sana kufa .,may i die an old grandma Amen..
 
ndo mana tunaambiwa to live it to the fullest ,with love and doing what u want ,mana anything can happen at any time...kila nikiwaza daaah,naogopa sana kufa .,may i die an old grandma Amen..
wewe umeua bend kabisa!
 
This is Paranormal phenomena, kuna uwezekano kuwa ndege hii haijaanguka wala haijatekwa, abiria wote wako hai somewhere
chances are slim kwa wao kuwa hai...am convinced it's somewhere in a trench huko baharini...maybe Mariana's trench
 
Yote yanawezekana hakuna kumuamini mmarekani kila taifa linajitegemea lakini pia tunasaidiana kama binadamu. Inawezekana imeanguka kwenye milima ya Uzbekistan au baharini nobody knows kwani ndege nyingi zimepotea bila kujulikana kama ya air India iliyoanguka France ilipatikana baada ya miaka 50. Lakini kwa hali iliyopo sasa na ubabe wa mmarekani anything can happen
 
okey! kwani haya masetelite hayafanyi kazi? mbona wamarekani waliweza kumuua Osama bila Pakistan kujua? yaani kwa dunia ya sasa (kitechnolojia) wenzetu wako mbali sana, sasa sijui setilite zao zilizimwa au ...sipati picha
 
Mungu anajua kwani huwa wanatabiri hali ya hewa kuwa swari halafu gharika inawakumba kwa hiyo basi ndugu yangu mi namuamini muumba wa vyote na kila analotaka liwe linakuwa asante
 
Back
Top Bottom