Dunia Ni Hadaa, Ulimwengu Ni Shujaa.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,790
Kuna wanawake unaweza kusema walipendelewa wakati wa uumbaji. Mafano wa wanawake hao alikuwa jirani yetu tukiwa wadogo. Tuliishi kwenye flats, yule mama alikuwa next door neighbour. Alipangiwa flat ile na mhindi aliyekuwa tajiri sana na alimiliki kampuni kubwa tu ya kuingiza magari miaka ile. Inavyosemekana mhindi yule alikutana na yule mama huko mkoani, alizubaishwa na uzuri wa yule mama alihakikisha anampatia flat aliweka furniture zote za ndani kabla hajamleta. Tukiwa wadogo tulipenda sana kwenda kwenye ile nyumba, ilikuwa safi, ushamba wa utoto tena, tuliona ajabu kukuta carpet mpaka chooni.

Yule mhindi alikuwa anakujaga pale anakaa siku siku kadhaa bila hata kutoka nje, watoto wake wakiume wakubwa walijua baba yao alipo na kama kulikuwa na document za muhimu zinataka sahihi ya mzee wao walikuja pale na baba akazipitia na kutoa sahihi. Wakati huo alimuaga mkewe amesafiri.

Yule mama hakutakiwa kuleta mtu yeyote pale, ingawaje alisaidia sana watoto wa ndugu zake kutoka kijijini, wakifika mjini aliwapangishia vyumba na kuwasaidia kwa siku za kwanza. Nisikiavyo alikuwa akipata ujauzito tu mzee anampeleka Nairobi, mimba inatolewa.

Mhindi akiwa safarini alikutusanya watoto wote wa rika letu pale maflatini either mnapewa soda na cake/biscuits, mnapelekwa Oysterbay beach/Msasani beach au mnapelekwa Avalon, Empire au Empress kuangalia movie na kula ice cream. Alipenda sana watoto.

Ikatokoea yule mhindi alifariki. Nisikiavyo alimuandikia yule mama mirathi lakini watoto wake wa kiume walihakikisha yule mama hapati kitu chochote tena walimtoa kabisa katika maisha yao.

Wakati huo sisi tulishahama pale maflatini, lakini yule mama alishindwa kuendelea kukaa pale, ukumbuke ni miaka ya awamu ya kwanza. Sikufahamu maisha yake yaliendeleaje, lakini nilipata habari anaumwa sana, wale watoto wa ndugu aliowasaidia hawakumjali kabisa, ni mmoja tu ndiye alikaa nae. Tulipopata taarifa tulitafutana watoto wote aliotupa good time enzi zake, tulijichangisha hela na kumsaidia mpaka mauti yalipomkuta.

Ninaandika hii habari huku machozi yakinitoka.
 
Basi pole Sky Eclat baby,usilie mamiii utaniliza na mimi.
 
Back
Top Bottom