Maguge Maguge
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 2,734
- 1,778
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia:
1.Mifereji huko Verdun (Ufaransa) baada ya kulimwa kwa mizinga mikubwa;
2. Ndege za kijeshi na faru za kwanza;
3. bunduki ya mtombo na manowari
Ramani ya dunia ikionyesha nchi na maeneo yaliyoshiriki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kijani: Mataifa ya Ushirikiano; njano: Mataifa ya Kati; nchi zisizoshiriki kwa rangi ya kijivu
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwaUjerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria naUturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati") kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi,Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano").
Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika naAsia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.
Sababu na matokeo
Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzikatika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wakikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.
Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Ufini, Latvia,Estonia na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria,Hungaria, Lithuania na Poland.
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita kuanzia 1939 hadi 1945 ya Ujerumani,Italia, Japani na mataifa yaliyoshikamana nao (Romania,Hungaria na Bulgaria) dhidi ya nchi nyingi za dunia (ziliitwa mataifa ya ushirikiano) kati yao hasa Uingereza,Uchina, Urusi na Marekani.
mapambano haya yalikuwa kati ya Ujerumani na wenzake dhidi ya nchi nyingi. Vita ya 1914/1918 iliitwa "Vita Kuu ya Dunia" kwa sababu mapigano yalienea pande nyingi za dunia yote tofauti na vita zilizotangulia. Kwa namna fulani vita iliyoanza 1939ilikuwa marudio ya vita iliyotangulia. Hivyo imekuwa kawaida kuzitaja vita hizi kama Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.
Mwanzo wa vita
Vita hii ilianza huko Ulaya tarehe 1 Septemba 1939 kwa mashambulizi ya Wajerumani dhidi Poland. Wengine huhesabu mashambulizi ya Japani dhidiUchina tarehe 7 Julai 1937 kuwa mwanzo wa vita. Mwisho wake ulikuwa huko Ulaya tarehe 9 Mei 1945 halafu huko Asia tarehe 2 Septemba 1945.
Mataifa ya ushirikiano
Mataifa ya Dunia wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia;
Njano-dhahabu: Ujerumani, Italia, Japani na nchi zilizoshikamana nazo; Kijani cheusi: Mataifa ya ushirikiano kabla ya Desemba 1941 (Pearl Harbour); Kijani kibichi: Mataifa yaliyojiunga na ushirikiano tangu Pearl Harbour hadi 1945
Mataifa ya ushirikiano (Kiing.: Allied powers, Allies of WW II) ni jina la kutaja mataifa yaliyoungana pamoja dhidi yaUjerumani na nchi zilizoshikamana nayo hasa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Duniana pia wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Ujerumani ilishambulia Poland tarehe 1 Septemba 1939. Ufaransa na Uingerezaziliwahi kutia saini mikataba ya ulinzi pamoja na Poland hivyo zilitangaza hali ya vita dhidi ya Ujerumani. Kanada,Australia, New Zealand na Afrika Kusinizilizokuwa nchi huru ndani ya British Commonwealth zilifuata zikatangaza vita dhidi ya Ujerumani katika siku za kwanza za Septemba 1939.
Ufaransa na Uingereza zilikuwa pamoja na maeneo ya koloni zao na hivyo sehemu kubwa ya eneo la dunia lilijumlishwa tayari katika juhudi za mataifa ya ushirikiano. Ni hasa Uhindi wa Kiingereza (Uhindi, Pakistan naBangla Desh leo) iliyochangia mali na watu wengi katika vita. Maaskari waafrika kutoka majeshi ya kikoloni waliungwa pia na juhudi hizi.
Baada ya mashambulio ya Ujerumani dhidi ya Denmark, Norwei, Ubelgiji na Uholanzi nchi hizi zilitazamiwa kama sehemu ya mataifa ya ushirikiano hata kama yalitekwa na kutawaliwa na Ujerumani.
Mwaka 1941 iliona vita ya Ujerumani naItalia dhidi ya Umoja wa Kisovyeti(Urusi) na nchi za Ulaya kusini-mashariki kama Ugiriki na Yugoslavia. Marekani ilikuwa bado nje ya vita lakini serikali yake ilitoa tayari misaada mingi kwa Uingereza.
Mwezi wa Novemba 1941 viongozi wa nchi kubwa Franklin D. Roosevelt(Marekani), Winston Churchill (Ufalme wa Maungano- Uingereza) na Stalin(Umoja wa Kisovyeti - Urusi) walikutana mjini Teheran (Uajemi) wakajadili ushirikiano wao na mipango ya vita.
Tarehe 7 Desemba 1941 Japan ilishambulia bandari ya kimarekani yaPearl Harbour, Hawaii. Ujerumani ilitangaza hali ya vita dhidi ya Marekani. Tangu hapo nchi nyingi za Amerika yote zilijiunga na mataifa ya ushirikiano. Mwisho wa vita nchi zote za dunia isipokuwa Hispania, Ureno, Uswidi, Uswisi, Eire, Afghanistan, Tibet zilijiunga na mataifa ya ushirikiano dhidi ya Ujeruman, Japani, Hungaria na Bulgaria. Italia ilikuwa ilijitenga tayari 1943 na Ujerumani isipokuwa sehemu kubwa bado ilikuwa chini ya utawala wa jeshi la Ujerumani.
Ushirikiano huu ulikuwa chanzo chaUmoja wa Mataifa ulioundwa mwaka1945 mara baada ya mwisho wa vita.
Kwa rekodi hii maana yake ni kwamba, Mataifa mawili yenye nguvu ndiyo yaliyosababisha vita ya kwanza ya Dunia, na hata ya pili nayo kadhalika.