Dunia inatafsiri kutoa kama kupata

Dunia inatafsiri kutoa kama kupata

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,735
Reaction score
4,933
KUTOA NI KANUNI YA ASILI YA ULIMWENGU INAYOMAANISHA KUPATA.

Hakuna kiumbe kinachoweza kukwepa kupata. Kupata hapa namaanisha kukidhi mahitaji ya kuendelea kuwepo na pia kuongezeka. Hii ni kanuni ya asili na unapoifuata kwa kujua au kutokujua matokeo yake ni kupata.

Kutoa siyo kupoteza katika Kanuni hii ila kutoa ni kupanda ili kupata. Hakuna kinachopatikana Duniani bila kutoa kitu kingine. Ni mtazamo potofu tu wa Mwanadamu kuamini katika kupata na kusahau mchakato wa kupata.

Dunia inatafsiri kutoa na kupokea kama kitu kilekile kimoja lakini akili ya Mwanadamu inatofautisha kutoa na kupokea kama vitu tofauti. Baadhi ya akili za watu zilizougundua ukweli huu ni akili ya Albert Einstern aliyeitwa wa ukinyume.
 
Back
Top Bottom