Duhh! Mambo mseto Radio One kuna mambo kweli,Na kama ni KWL mbona ni ISHU! Nina shaka

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Nikiwa nyumbani nikiwa najiliwaza kwa hili na lile baada ya kutoka church,nikafungulia Radio One mambo mseto na ndipo nikapata kumsikiliza yule mtangazaji wa radio one toka Morogoro akitoa vihoja ya kweli toka huko mkoani Moro na akimimina aliyoyaona baada driver wa lori moja waliokuwa wanasafiri naye na konda wake kupaki na wakateremka kwenda kupata moja baridi na moja moto na ndipo walipomaliza na kurudi kwenye gari na kujaribu kuwasha bila ya mafanikio konda naye akajaribu kuwasha bila ya kuwaka na ndipo wakafikia maamuzi ya kumtafuta fundi naye akaja akajaribu kulikagua gari akasema haoni tatizo na ndipo wakabaki wakiduwaa bila ya kujua la kufanya na ndipo wakapiga simu kwa office na akaja fundi wa kampuni lengwa la gari naye akajaribu kulikagua naye haoni tatizo,na ndipo akagundua ya kwamba dereva na konda wake wote wamelewa na ndipo akaingia mwenyewe na kuliwasha na gari likakubali na safari ikaendelea. Swali! Mi nafikiri hilo gari ni la Kichina maana mtangazaji ajasema ni aina gani zaidi ya kusema lori,kwanini yasiletwe mengi hapa Nchi na ajali mbona ingepungua? Ama kama ni chombo cha kufunga kwenye magari,si ingefungwa ktk magari madogo na makubwa kana kwmb driver akigusa tu ingali amekunywa pombe na gari hata lisifunguke mlango licha ya kuwaka. Mi ningependa hili sana! Ni hayo tu wanaJF na niwatakieni J'pili njema. Source Radio One:
 
Mara nyingi mambo mseto huongea kisa mkasa. Ni mambo ya kweli, lakini la gari...nahofia. Ila pia technologia ikiwa kubwa ni rahisi kuweka censor ya alcohol na kuzuia gari kuwaka. But ....
Hivi huu mkasa wa kweli au ndo mambo mseto?
 
Hiyo stori ina ukweli na uongo.

UKWELI.
Kuna alcohol sensor ambazo kama dereva umefikia kiwango fulani cha kilevi gari hailitawaka.

UONGO.
Vifaa hivyo ni mpaka ukipumulie. [breathalyzer] angalia hapa Alcohol Breathalyzer | Portable and Handheld Breathalyzer Testing.
Sasa haiwezekani uingie tu kwenye gari uwashe na lisiwake kwa kuwa umelewa. Gari litakataa kuwaka endapo tu umepima na kiwango cha kilevi cha mtumiaji kimezidi kiwango kinachotatikana. Na stori hii haijasema kwamba kuna kifaa kama hicho walipulizia.
 
Kweli yule msemaji toka pale mji kasoro bahari (MORO) hajasema kama kuna ki2 cha kupumulia ila nataka kusema ya kwmb kama kuna mtu yeyote mwenye mawasiliano yake anijuze na niseme naye halafu niweze kujuza umma kwa undani maana kama hili linawezekana Mi ninaona ni issue sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom