Duh! Kumbe Yanga ilimsubiri Tambwe bandarini

Duh! Kumbe Yanga ilimsubiri Tambwe bandarini

Joined
Sep 3, 2014
Posts
11
Reaction score
3
Share
YANGA kumbe wajanja sana kwani walikuwa wanaisikilizia Simba kama ingemtema straika Amissi Tambwe tu, fasta ingemsubiri bandarini Dar es Salaam na kumsajili kwa dau la Sh48.7 milioni kisha ingemtema Genilson Santos Jaja.

Baada ya kumjumuisha kikosini mwake, Emmanuel Okwi, Simba ilitakiwa kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni ambapo Kocha Patrick Phiri alikuwa na mpango wa kumkata Tambwe na kumwacha Donald Mosoti ili kuimarisha safu ya ulinzi.

Lakini uongozi wa Simba uliketi na Phiri na kuamua kuachana na Mosoti kwa hesabu kwamba Tambwe aliisaidia timu msimu uliopita hata kuwa Mfungaji Bora kwa mabao 19 aliyofunga, hivyo ingekuwa vigumu kuachana naye.

Wakati Simba wakijadiliana, viongozi wa Yanga walikuwa wametega masikio yao kusikilizia endapo Tambwe angetupiwa virago tu basi haraka wangemsajili kwa dau la dola 30,000 sawa na Sh48.7 milioni kuimarisha kikosi chake.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye ana kauli nzito kwenye mambo ya usajili aliliambia Mwanaspoti kuwa, walipata habari za kuachwa kwa Tambwe .
 
Hii itaendelea kuwa ni soga tu
 
Kikosi cha kwanza cha Yanga,wachezaj 7 wametokea simba,huu ni ushenz wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom