Dongeee hilo, hamna lolote. Swali limeulizwa sula la Dual citizenship limefikia wapi. Unachojibu ni nje ya mada husika kabisa. Yaonyesha elimu haikusidii wewe hata tonye. Ndio nyie nyie!Rudi nyumbani uwasaidie watanzania wenzako,uraia wa nchi mbili kwangu ni upuuzi mtupu,tutaiga wazungu kila kitu? wao wanafanya hivyo ili wapate nafasi ya kuhujumu.
Asante sana Kiongozi, ila huyu Mhe. Membe naye haelewi hata tonye. Kuwa na uraia wa nchi mbili haimanishi kuwa umeusaliti mwingine haswa ule wako wa kuzaliwa. kila nchi ina masharti yake na ndio maana ukiwana dual citizenship kama wewe si mzawa wa hiyo nchi basi kuna nafasi fulani fulani za serikali huwezi kugombania au kupewa. Mfano wewe ni mzaliwa wa Tanzania na una dual citizenship ya Tanzania na Uturuki ina maana huwezi kuwa katika nafasi fulani fulani za nchi ya Uturuki ila kwa Tanzania unaweza kwa sababu wewe ni mzaliwa wa nchi hiyo.Lakini nimemuona Mhe Bernard Membe akisema kuwa uraia wa kuzaliwa hakuna anaeweza kuufuta na hivyo ndivyo inavyotambulika na hao dunia ya kwanza, sasa wale wenzetu waliochukua uraia wa nchi nyengine kwa kuandikisha si raia wa Tanzania kwa kuzaliwa? Moja na moja ni mbili au vipi?
Hongera sana kwa hilo. Kila mtu ana mawazo yake na nadhani hapo ndipo mwisho yalipofikia yako ktk suala zima la dual citizenship. Kabla hata ya kuondokaga Tanzania nilishaonaga kuwa curriculum ya Tanzania inahitaji kubadilisha ili iboreshwe zaidi na pia iwe na michezo ndani yake. hii yote ni baada ya kuona wenzetu Uganda na kenya wakati nasoma katika nchi hizo miaka tofauti ya nyuma. Kiongozi husikurupuke kuchangia bila kuhoji baadhi ya mambo muhimu kwa undani zaidi.safi sana mkuu, umenikuna mpaka natoka unga. itabidi nikugongee thanks.
mtu mzima hataki kurudi nyumbani anabangaiza apate uraia wa nchi nyoingine utadhani hana nchi yake. hawa ndio wanaotutia aibu huku ng'ambo. nikipata nafasi ya maamuzi siku moja msahau kabisa huyo punda anayeitwa uraia wa nchi mbili.
mi niko ng'ambo kwa sasa naingia na kutoka karibu kila nchi ninayotaka bila matatizo ya kunyimwa au kucheleweshewa viza na nina uhakika wa kuendelea kukaa huku niliko (kama nitataka) ng'ambo kwa muda wote nitakaopenda. lakini uraia wa nchi tofauti na tanzania hata ukiniletea bure kwenye karai sichukui. upuuuzi mtupu.
nimetembea sana dunia sijaona nchi nzuri kama tanzania! jamani watanzania turudi nyumbani tujenge nchi yetu, sio mkae huku mkiuliza tanzania imewafanyia nini mje kula.
mimi narudi februari mwakani.
jamani kila anyetaka kurudi aandike hapa anarudi lini sio huu upuuzi wa dual citizenship!.
Unafikiri kuwa Tanzania ndiyo kuipenda Tanzania?
I wish Lowassa na kundi lake la Mafisadi wangelikuwa wanaishi nje.
Anyway, Utanzania uko moyoni mwa mtu na siyo kwenye JF au kurudi Tanzania. Hata Boss wa Marks and Spencer aitwaye Stuart Rose ambaye alishawahi kuishi zamani Dodoma, alirudi huko na kusaidia shule ambapo zamani walikuwa wanakaa. Huyu ingawa si Raia wa Tanzania (na wala hahitaji) anaweza kuwa Mtanzania zaidi ya akina Lowassa, Mkapa, Liyumba, Mgonja, Mramba na wengine wengi tu.
Mwisho niseme kimoja. Nashindwa kufahamu unachokisema hapa wewe ni kuipenda Tanzania au Uraia wa nchi mbili? Je mtu mwenye uraia wa nchi mbili, ina maana haipendi Tanzania? Mwenye wa nchi moja na anaishi Tanzania ina maana anaipenda sana Tanzania?
Kwangu mie kuipenda Tanzania ni kama ule mfano wa tembo na vipofu 7. Kila mtu anagusa kipande fulani na anaonyesha mapenzi yake. Ukianza kuwacheka wanzako kwa kuonyesha mapenzi kwa Tanzania kwa njia nyingine tofauti na unazotaka wewe ndiyo hiyo ninasema kuwa Mkuu wewe una UMIMI SANA. Kwa nini unapoteza muda kwenye nchi za watu? Kaa Tanzania hadi uje ufie hapa. Una Passport yenye kukuruhusu kutembea dunia nzima na mwisho unakuja kudai watu WARUDI Tanzania. Wewe hiyo Passport na hizo VISA zilizomo ndani za nini?
http://www.youtube.com/watch?v=t3vJ...E50EFE27A&playnext=1&playnext_from=PL&index=6
Hongera sana kwa hilo. Kila mtu ana mawazo yake na nadhani hapo ndipo mwisho yalipofikia yako ktk suala zima la dual citizenship. Kabla hata ya kuondokaga Tanzania nilishaonaga kuwa curriculum ya Tanzania inahitaji kubadilisha ili iboreshwe zaidi na pia iwe na michezo ndani yake. hii yote ni baada ya kuona wenzetu Uganda na kenya wakati nasoma katika nchi hizo miaka tofauti ya nyuma. Kiongozi husikurupuke kuchangia bila kuhoji baadhi ya mambo muhimu kwa undani zaidi.