wewe ni jahil muraqqabu, Acha wizi bora kulima kuliko kuishi kwa ujanja...
ﺑَﺎﺏُ ﻣَﺎ ﺟَﺎﺀَ ﻓِﻲ ﺍﻟْﻜُﻬَّﺎﻥِ ﻭَﻧَﺤْﻮِﻫِﻢْ
Kuhusu Makuhani Na Mfano Wao
ﺭَﻭَﻯ ﻣُﺴْﻠِﻢٌ ﻓِﻲ ﺻَﺤِﻴﺤِﻪِ ﻋَﻦْ ﺑَﻌْﺾِ ﺃَﺯْﻭَﺍﺝِ ﺍﻟﻨَّﺒِﻲِّ ( ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ ) ﻋَﻦِ ﺍﻟﻨَّﺒِﻲِّ ( ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ ) ﻗَﺎﻝَ : )) ﻣَﻦْ ﺃَﺗَﻰ ﻋَﺮَّﺍﻓًﺎ ﻓَﺴَﺄَﻟَﻪُ ﻋَﻦْ ﺷَﻲْﺀٍ ﻓَﺼَﺪَّﻗَﻪُ، ﻟَﻢْ ﺗُﻘْﺒَﻞْ ﻟَﻪُ ﺻَﻼﺓٌ ﺃَﺭْﺑَﻌِﻴﻦَ ﻳَﻮْﻣًﺎ ((
Amesimulia Muslim katika Swahiyh yake kutoka baadhi ya wake wa Nabiy ( ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ ) kwamba Nabiy ( ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ ) amesema: ((Atakayemwendea mtabiri akamuuliza kitu kisha akamuamini, haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini))
[Muslim]
ﻭَﻋَﻦْ ﺃَﺑِﻲ ﻫُﺮَﻳْﺮَﺓَ ( ﺭَﺿِﻲَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻨْﻪُ ) ﻋَﻦِ ﺍﻟﻨَّﺒِﻲِّ ( ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ )
ﻗَﺎﻝَ : )) ﻣَﻦْ ﺃَﺗَﻰ ﻛَﺎﻫِﻨًﺎ، ﻓَﺼَﺪَّﻗَﻪُ ﺑِﻤَﺎ ﻳَﻘُﻮﻝُ ﻓَﻘَﺪْ ﻛَﻔَﺮَ ﺑِﻤَﺎ ﺃُﻧْﺰِﻝَ ﻋَﻠَﻰ ﻣُﺤَﻤَّﺪٍ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ (( ﺭَﻭَﺍﻩُ ﺃَﺑُﻮ ﺩَﺍﻭُﺩَ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah ( ﺭَﺿِﻲَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻨْﻪُ ) kutoka kwa Nabiy ( ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ ) amesema:
((Atakayemkaribia kuhani na kuamini anayoyasema basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ )) [Abuu Daawuwd]
ﻭَﻟِﻸَﺭْﺑَﻌَﺔِ ﻭَﺍﻟْﺤَﺎﻛِﻢِ ﻭَﻗَﺎﻝَ : ﺻَﺤِﻴﺢٌ ﻋَﻠَﻰ ﺷَﺮْﻃِﻬِﻤَﺎ ﻋَﻦْ ﺃَﺑِﻲ ﻫُﺮَﻳْﺮَﺓَ : )) ﻣَﻦْ ﺃَﺗَﻰ ﻋَﺮَّﺍﻓًﺎ ﺃَﻭْ ﻛَﺎﻫِﻨًﺎ ﻓَﺼَﺪَّﻗَﻪُ ﺑِﻤَﺎ ﻳَﻘُﻮﻝُ ﻓَﻘَﺪْ
ﻛَﻔَﺮَ ﺑِﻤَﺎ ﺃُﻧْﺰِﻝَ ﻋَﻠَﻰ ﻣُﺤَﻤَّﺪٍ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ ((
Na wasimuliaji wengine wanne wa Hadiyth na Al-Haakim wamenakilii Hadiyth ya Abuu Hurayrah( ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ) na wameikiri ni Swahiyh kwa mujibu wa masharti yao kwamba: ((Atakayemwendea m tabiri au kuhani akamwamini ayasemayo basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ ))
ﻭَﻷَﺑِﻲ ﻳَﻌَﻠَﻰ ﺑِﺴَﻨَﺪٍ ﺟَﻴِّﺪٍ ﻋَﻦِ ﺍﺑْﻦِ ﻣَﺴْﻌُﻮﺩٍ ﻣِﺜْﻠُﻪُ ﻣَﻮْﻗُﻮﻓًﺎ
Na Abuu Ya’laa ameripoti Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Ibn Mas’uwd kwa isnaad nzuri lakini ni Hadiyth Mawquwf.
ﻭَﻋَﻦْ ﻋِﻤْﺮَﺍﻥَ ﺑْﻦِ ﺣُﺼَﻴﻦٍ ﻣَﺮْﻓُﻮﻋًﺎ : )) ﻟَﻴْﺲَ ﻣِﻨَّﺎ ﻣَﻦْ ﺗَﻄَﻴَّﺮَ ﺃَﻭْ ﺗُﻄُﻴِّﺮَ ﻟَﻪُ، ﺃَﻭْ ﺗَﻜَﻬَّﻦَ ﺃَﻭْ ﺗُﻜُﻬِّﻦَ ﻟَﻪُ، ﺃَﻭْ ﺳَﺤَﺮَ ﺃَﻭْ ﺳُﺤِﺮَ ﻟَﻪُ، ﻭَﻣَﻦْ ﺃَﺗَﻰ ﻛَﺎﻫِﻨًﺎ ﻓَﺼَﺪَّﻗَﻪُ ﺑِﻤَﺎ ﻳَﻘُﻮﻝُ، ﻓَﻘَﺪْ ﻛَﻔَﺮَ ﺑِﻤَﺎ ﺃُﻧْﺰِﻝَ ﻋَﻠَﻰ ﻣُﺤَﻤَّﺪٍ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ (( ﺭَﻭَﺍﻩُ ﺍﻟْﺒَﺰَّﺍﺭُ ﺑِﺈِﺳْﻨَﺎﺩٍ ﺟَﻴِّﺪٍ
Na Imepokelewa toka kwa ‘Imraan bin Huswayn Hadiyth Marfuw’: ((Si miongoni mwetu anayetafuta au anayebashiriwa Atw-Twiyaarah (mkosi, nuksi) au akafanya ukuhani au akafanyiwa ukuhani, au anayefanya uchawi au anayefanyiwa uchawi, na atakayemwendea kuhani
akamwamini ayasemayo basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ )) [Al-Bazaar kwa isnaad nzuri]
ﻭَﺭَﻭَﺍﻩُ ﺍﻟﻄَّﺒَﺮَﺍﻧِﻲُّ ﻓِﻲ ﺍﻟْﺄَﻭْﺳَﻂِ ﺑِﺈِﺳْﻨَﺎﺩٍ ﺣَﺴَﻦٍ ﻣِﻦْ ﺣَﺪِﻳﺚِ ﺍﺑْﻦِ ﻋَﺒَّﺎﺱٍ ﺩُﻭﻥَ ﻗَﻮْﻟِﻪِ : )) ﻭَﻣَﻦْ ﺃَﺗَﻰ (( .. ﺇِﻟَﻰ ﺁﺧِﺮِﻩِ
Hadiyth hiyo hiyo ameinakili Atw-Twabaraaniy katika Al-Awsatw kwa isnaad nzuri kutoka kwa Ibn ‘Abbaas bila ya kauli ya mwisho: ((Na atakayemwendea…))
ﻗَﺎﻝَ ﺍﻟْﺒَﻐَﻮِﻱُّ : ﺍﻟْﻌَﺮَّﺍﻑُ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﻳَﺪَّﻋِﻲ ﻣَﻌْﺮِﻓَﺔَ ﺍﻷُﻣُﻮﺭِ ﺑِﻤُﻘَﺪِّﻣَﺎﺕٍ ﻳُﺴْﺘَﺪَﻝُّ ﺑِﻬَﺎ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟْﻤَﺴْﺮُﻭﻕِ ﻭَﻣَﻜَﺎﻥِ ﺍﻟﻀَّﺎﻟَّﺔِ ﻭَﻧَﺤْﻮِ ﺫَﻟِﻚَ
Al-Baghaawiy amesema: Al-‘Arraaf (mtabiri) ni ambaye anadai ujuzi wa mambo fulani kama vile yanayohusu vitu vilivyoibiwa, wapi vipo vitu hivyo, au mnyama aliyepotea na kama hayo kwa njia ya uchawi.
ﻭَﻗِﻴﻞَ ﻫُﻮَ ﺍﻟْﻜَﺎﻫِﻦُ، ﻭَﺍﻟْﻜَﺎﻫِﻦُ ﻫُﻮَ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﻳُﺨْﺒِﺮُ ﻋَﻦِ ﺍﻟْﻤُﻐَﻴَّﺒَﺎﺕِ ﻓِﻲ ﺍﻟْﻤُﺴْﺘَﻘْﺒَﻞِ
Wengine wamesema yeye ndiye kuhani, na kuhani ni anayetoa khabari za mustaqbal (za mbele) zilizofichikana.
ﻭَﻗِﻴﻞَ ﺍﻟَّﺬِﻱ ﻳُﺨْﺒِﺮُ ﻋَﻤَّﺎ ﻓِﻲ ﺍﻟﻀَّﻤِﻴﺮِ
Na wengine wamesema ni ambaye anayetoa yaliyo katika dhamira ya mtu (siri moyoni).
ﻭَﻗَﺎﻝَ ﺃَﺑُﻮ ﺍﻟْﻌَﺒَّﺎﺱِ ﺍﺑْﻦُ ﺗَﻴْﻤِﻴَّﺔَ ﺍﻟْﻌَﺮَّﺍﻑُ ﺍﺳْﻢٌ ﻟِﻠْﻜَﺎﻫِﻦِ، ﻭَﺍﻟْﻤُﻨَﺠِّﻢِ ﻭَﺍﻟﺮَّﻣَّﺎﻝِ
ﻭَﻧَﺤْﻮِﻫِﻢْ ﻣِﻤَّﻦْ ﻳَﺘَﻜَﻠَّﻢُ ﻓِﻲ ﻣَﻌْﺮِﻓَﺔِ ﺍﻷُﻣُﻮﺭِ ﺑِﻬَﺬِﻩِ ﺍﻟﻄُّﺮُﻕِ
Na Abul-‘Abbaas, Ibn Taymiyyah kasema: Al-‘Arraaf ni jina la kuhani, na Al-Munajjim (mtabiri wa nyota) na Ar-Rammaal (mpiga ramli) na kama hao wanaojidai kuyajua mambo kwa njia hizo.
ﻭَﻗَﺎﻝَ ﺍﺑْﻦُ ﻋَﺒَّﺎﺱٍ ﻓِﻲ ﻗَﻮْﻡٍ ﻳَﻜْﺘُﺒُﻮﻥَ : ﺃَﺑَﺎ ﺟَﺎﺩٍ . ﻭَﻳَﻨْﻈُﺮُﻭﻥَ ﻓِﻲ ﺍﻟﻨُّﺠُﻮﻡِ ﻣَﺎ ﺃَﺭَﻯ ﻣَﻦْ ﻓَﻌَﻞَ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﻪُ ﻋِﻨْﺪَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻣِﻦْ ﺧَﻼﻕٍ
Na Ibn ‘Abbaas akasema kuhusu watu wanaoandika ‘Abaa-Jaad’ (alfabeti kutumilia utabiri, uaguzi) na wanatazamia nyota kuamini athari zake ardhini. “Sioni kuwa wana fungu lolote mbele ya Allaah.”
.........NJOO UJIBU KAMA UNAJIWEZA KIELIMU SIO UNABAKI NA HOJA ZAKUBAMBANYA