Dua ninayoiombea Nchi yetu leo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dua ninayoiombea Nchi yetu leo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Mchungaji, Jul 5, 2012.

 1. B

  Baba Mchungaji Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baba yetu uliye mbinguni asante kwa kunipatia uzima na afya asante kwa kunipatia kibari cha kufanya maombi haya! Nakushukuru kwakuwa wewe wanipenda sana pia unaipenda nchi yetu ya tanzania mungu tunakushukuru kwa neema uliyotujaaria katika taifa letu tunakushukuru kwa upendo wako wa ukweli unaouotufanyia, nakuomba utusamehe makosa yetu tuliyokukosea kwa kuwaza, kunena, kutenda na hata kwa kutokutimiza wajibu! Nakuomba utusamehe na kuturehemu kwa rehema yako iliyo kuu! Nakushukuru kwakuwa wewe ni mungu uliye mwaminifu kwakuwa umeahidi ya kuwa tukiomba msamaha utatusamehe kama ulivyo wasamehe daudi, samsoni na wengine wengi, nakuomba uwasamehe hata wale walionikosea kwa kujua au kwa kutokujua kwakuwa mie wote nimekwisha wasamehe naomba unisamehe na mimi ee mungu wangu na unitakase kwa damu ya yesu! Ahsante bwana wa majeshi, nakusihi mungu uwabariki viongozi wetu, na uwabariki wale wote wanaotutakia mema wanachi wa taifa hili, pia wasaidie viongozi wetu kuanzia rais wetu mpaka wenyeviti wa mtaa, pia nakuomba uwasaidie wabunge wa nchi yetu ambao wapo kwenye vikao vya bajeti na kuwaondolea roho ya ubinafsi ili waweze kuwawakilisha vyema wananchi wote, nakuomba ee baba yangu uwasaidie wajumbe wa kamati ya katiba ili wakusanye maoni ambayo yatatusaidia kuunda katiba itakayokuwa inaangalia masilahi ya taifa siyo kikundi cha watu wachache! Mungu wangu naamini yote niyaombayo utatenda kwakuwa mala zote nikikuomba wewe hujibu nakuomba uwasaidie sana viongozi wote wakujue wewe mungu wa ukweli na wa pekee usiye fananishwa ili wakapate kutenda sawasawa na mapenzi yako, nakuomba mungu viongozi wote wezi uwaaibishe kwakuwa wewe ni muweza wa yote naamini yote yanawezekana kwako! Naliinua jina lako ee yesu uliye mwana wa pekee wa mungu na mjumbe wa agano jipya, nakusihi ee baba yangu wa mbinguni uilinde nchi yetu kwakuwa wewe umesema bwana asipoilinda nyumba alindaye akesha bure! Nakuomba uilinde nchi yetu ili iwe salama daima katika jina la bwana wetu yesu kristo unayestahili sifa na heshima naomba na kushukuru amen!.
   
 2. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ameen!
   
Loading...