Dua! Damu ya Mtz ikimwagika kwasababu ya kudai Katiba ya Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dua! Damu ya Mtz ikimwagika kwasababu ya kudai Katiba ya Wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Nov 29, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Baada ya wabunge wa CCM,CUF na TLP kuwasimanga na kuwatukana wabunge wa CHADEMA na NCCR, Kikwete kuipuuza Kamati ya CHADEMA, na Serikali kukidharau kilio cha umma wa Watanganyika. Ndipo nikaenda katika uwanja wa fikra huru, nikasimama panapo jukwaa la haki nikiziegemea nguzo mbili, moja waliita USAWA na ya pili waliita UTU (wakimaanisha thamani ya utu) ambapo mbele yake palikuwa na meza ya zamani ya mvule iliyofunikwa kitambaa cha samawati kikiwa na maandishi mekundu

  " Wana wa Tanganyika, wa makabila yalo changanyika,
  Waliozaliwa Tanganyika, Mola ndo kawasimika,
  Uhai wao kutunzwa, sii jambo la kupuuzwa"

  Ndipo nikainua kichwa changu juu mawinguni na kuomba dua mbele zake Muumba nikisema,

  "Ee Mwenyezi Mungu, Mola wetu, mwenye haki. Ulitufanya tukazaliwa Tanganyika si kwa matakwa yetu bali mapenzi yako. Umeliona jambo hili la Katiba namna viongozi wetu walivyotutenda kwa dhuruma na maneno ya kejeli na kutimiliza kwa kutudharau. Basi sasa, ikiwa damu ya mtanganyika yeyote itamwagika kwasababu kudai Katiba ya Haki ya Wananchi kutakakofanywa na Serikali kwa kutumia Polisi ama vyovyote, twaomba ukatulipie kisasi cha damu hiyo juu ya Rais, waziri mkuu, spika, mawaziri wa sheria, mwanasheria mkuu na wabunge wote walioruhusu udhalimu huu.

  Ulipokuwa mikononi mwao walikuwa na uwezo kuuzuia bali wao walichagua kutupa kinga cha moto ktk petroli na kukitukuza kiburi chao. Kwa jinsi ileile watanganyika watakavyolia kwa kupotelewa na mzazi wao, mtoto wao ama ndugu yao na wao pia wakalie.

  Ee Mola wetu, haki ina wewe, ndiwe mlipiza kisasi kwa ajili ya mnyonge. Damu hiyo ikawe juu yao.

  Twaomba ukatulipie kisasi. Amina"
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa dalili za kulipuka kwa maandamano zinazidi kujionyesha, suala la msingi si kupambana na maadamano bali na kiini cha maandamano ndipo tatizo litakuwa limetatuliwa.

  ukweli ni kuwa kitakacho wasukuma watu kuandamana si uwezo wao kipesa bali ni dhamira zao kutaka kuaj kuiona Tanganyika njema kwao na watoto wao na vizazi vingi baada yao vitakavyoishi Tanganyika ama vikitokea Tanganyika.
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mungu nisaidie na wewe unaweka nguvu zako.
  Hili la damu kumwagika halitakuwa geni sasa maana tumeona damu Arusha, Igunga, mbeya na wengine ambao 'wameunguzwa'
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ewe Mwenyezi Mungu wape ujasiri waja wako ili waweze kupigania haki yao na ya vizazi vyao vya baadae; pia uwafumbue akili hao mapolisi na wanajeshi watambue kuwa hao watakaoandamana ni baba zao,mama zao, dada zao na kaka zao na wanafanya hivyo kwa niaba yao ili maisha yao ya baadae yawe bora kuliko hivi sasa wanavyopigika!! Onyesha nguvu zako Mwenyezi hizo risasi kama zitarindima zisimpate mtu bali zigeuke kuwa maji ya kuoga!!
   
 5. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nchi hii bwana,,
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli ndugu yangu, kwamba halitakuwa geni. Lakini hatupendi litokee ikiwa ipo namna ya mapema ya kuzuia lisitokee; nayo ni kutotumia nguvu za Polisi au Jeshi, na kuifuta sheria mbovu ya Marekebisho ya Katiba ya 2011.

  Sasa, endapo hayo yatapuzwa kama yalivyopuu9a ya awali wananchi watatumia nguvu waliyonayo. Kutumia nguvu kwa kila upande kutarejeresha umwagaji mkubwa wa damu zisizo na hatia za watanganyika.. Ikiwa tunajua kuwa kila damu inayomwagika huwa inaomba mbele za Mungu, ilipiwe kisasi cha damu kwa walioimwaga. Kwanini tusiombe kisasi hicho toka kwa Mungu kisiwakute waliosabisha hayo (niliowataja hapo juu) na uzao wao?
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  amina!!
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Blood can buy peace.
  Blood can't buy peace.
   
Loading...