DSTV gharama ziko juu.. Kwanini..?

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
Wanabodi..
Najua tuko kwenye soko huria na bei inapangwa na watoa huduma (japo Serikali haikubali hili).. Lakini kulipa shilingi za kitanzania 128,000 kwa mwezi kwa ajili ya huduma za DSTV ni halali..? Pointi yangu hapa inarudi nyuma walipokuja kampuni ya Gtv (ambayo bahati mbaya ikafa kwenye anguko lile la uchumi duniani) waliweka ceilin price yao ambayo haikuzidi shs. 51,000..! Na hapo walikuwa wanaonyesha acilimia 80 ya mipira yote iliokuwa inaonyeshwa na DSTV.. Sasa kama wale wa Gtv waliweza kuweka kiaci hicho kidogo DSTV wanashindwa nini..? Au viongozi wanashindwa nini kuwalazimisha hawa kushusha fee yao ili wananchi wa kawaida nao waweze ku-afford..?

Kwenye usafiri wa anga wamekuja Fastjet.. Tunahitaji mkombozi kwenye sekta hii ya luninga..
 
HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
46,023
46,998
kwani dstv wako na package moja? Mbona mnapenda lalamika sana package zipo kuanzia 16000/= so uchaguzi ni wako hujalazimishwa kuweka premium na ndio maana ikaitwa premium. Hiyo unapata chanel zaidi ya 80 na za mpira unapata zote
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
unashangaa nini kwani hujui tanzania ni shamba la bibi viongozi ndio wenye hizo biashara.

Mkuu nilishambana kwa maswali Balozi Mpungwe kuhusu issue hii ya price.. Bt as usual akajifanya hauciki wakati I know ana hisa pale.. Yaani it irks me sana..!
 
Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,359
2,329
Kamata king'amuzi cha HAWK 777 kinatumia line ya gsm una subscribe bundle ya mwezi 2500 tshs then unakula fully channels za dstv mwezi mzima
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
kwani dstv wako na package moja? Mbona mnapenda lalamika sana package zipo kuanzia 16000/= so uchaguzi ni wako hujalazimishwa kuweka premium na ndio maana ikaitwa premium. Hiyo unapata chanel zaidi ya 80 na za mpira unapata zote

Unajua acilimia 90 wanaitaka DSTV kwa ajili ya kuangalia mipira..! Na ukitaka kujuab hilo subiri kipindi ambacho ligi zimeisha.. Hizo package unazozisema zina channel moja tu ya super sport tena kwa ajili ya mipira ya East Africa.. Swala sio kulazimishwa.. Swala ni haki kwa wasio na uwezo.. Ndio maana nikatoa mfano mbona Gtv walipokuja waliweka gharama chini..? Kwanini DSTV wawe juu kiaci hicho..?
 
englibertm

JF-Expert Member
May 1, 2009
9,255
6,205
Mkuu nilishambana kwa maswali Balozi Mpungwe kuhusu issue hii ya price.. Bt as usual akajifanya hauciki wakati I know ana hisa pale.. Yaani it irks me sana..!
nchi hii umejaa unafiki sana hawa viongozi wakiwa maajukwani utadhani malaika kumbe ni mashetani wakubwa
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
21,197
28,011
hahahah jamani gtv iliwaangusha wengi. wewe kununua rights toka kwa sky unadhani utani...lipia wewe. starehe gharama bwana
 
HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
46,023
46,998
sosoliso nadhani hizi bei zao ni kwa nchi nyingi maana huwa ni dollar 78 au 80
 
Last edited by a moderator:

Mzee wa fund

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
514
89
Tatizo la Dstv ni kwamba wana charge kwa $(dolla).hivyo gharama lazima iwe juu.pia thamani ya TSHS.vs$ ni ndogo sana.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,969
8,259
sosoliso nadhani hizi bei zao ni kwa nchi nyingi maana huwa ni dollar 78 au 80

Kwa point yako hii, mie nimejifunza kwamba tatizo ni shilingi yetu kushuka thamani ndio inafanya bei kuwa juu maana hiyo bei ya dola 78 imekaa muda mrefu lakini sie ndio kunakuwa na madiliko (wao ni dola 78 kwa mwaka mfululizo lakini sie kwa madafu yetu kunakuwa na bei tofauti 12 ktk miezi 12), nadhani tukomae shilingi ipande thamani
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
Kwa point yako hii, mie nimejifunza kwamba tatizo ni shilingi yetu kushuka thamani ndio inafanya bei kuwa juu maana hiyo bei ya dola 78 imekaa muda mrefu lakini sie ndio kunakuwa na madiliko (wao ni dola 78 kwa mwaka mfululizo lakini sie kwa madafu yetu kunakuwa na bei tofauti 12 ktk miezi 12), nadhani tukomae shilingi ipande thamani

Hapana Mkuu.. Kuweka kiwango cha dola ni mbinu ya makusudi ya kutufanya tufikirie sababu ya kuwa juu.. nitakupa mifano michache..
Kama unakumbuka makampuni ya cimu yalikuwa yanatuchaji muda wa hewani kwa kiwango cha dola.. Matokeo yake gharama ikawa inapanda kwa kuwa thamani ya shilingi yetu ilikuwa inashuka.. Lakini mbona walifanya uamuzi wa kuyaamuru mashirika hayo ya cimu kutoza kwa viwango vya shilingi.. Leo unaona gharama za cimu zilivyokuwa za chini.. Kama viwango vingebaki vya dola unadhani cimu zingekuwapo mpaka vijijini..?
Wanashindwa vipi kuwaamuru na hawa DSTV kuacha kutumia viwango vya dola..?
Halafu mbona Gtv waliweka flat rate ya Tanzania Shilings..? Mie ninaamini kwa hawa DSTV wanaweza kuweka kiwango cha hata Shs. 50,000 na wakapata faida kubwa.. Maana subscribers wataongezeka kwa kiwango kikubwa sana...
 
Tatizo viongozi wetu husema pasipo kutenda, wanapiga marufuku kulipa kwa dola na hapa wanajisifu matamko yao yamesikika kumbe kinachofanyika tunalipa kwa shilingi yetu kweli lakini kwa rate ya dola ya siku husika tena ya bei ya kununua dola wanachofanya wakipokea na wao wanaenda kuzibadilisha kuwa dola the same day
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom