A
Anonymous
Guest
Wakuu, nipo kitandani nikiugua, lakini roho inaniuma kuona jinsi uwekezaji wangu unavyoliwa na 'mchwa' mchana kweupe. Mimi ni mwekezaji (CDS No: 811....), nimeuza hisa mara nne ili nipate pesa za matibabu, lakini Vertex International Securities wameamua kunizungusha na kunitapeli.
Jana baada ya kelele nyingi, walidanganya DSE kuwa watalipa deni langu la 83,000/+, lakini wakatuma 16,448/- tu! Huu ni uhujumu uchumi na unyama dhidi ya mgonjwa. Lakini tatizo ni kubwa zaidi; Mifumo ya DSE imekuwa ikifeli na kuanguka kila siku, jambo linalosababisha pesa za wawekezaji kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Uzembe huu wa DSE na brokers wao umesababisha wawekezaji kulikimbia soko. Matokeo yake sasa soko limevamiwa na 'Panic Selling' ambapo kila mwekezaji anauza hisa na hakuna wanunuzi, hali inayopelekea hisa za makampuni makubwa kuporomoka thamani. Je, DSE mnasubiri mwekezaji afe kwa kukosa dawa ndipo mfanye kazi? Je, mnasubiri soko life kabisa?
Nahitaji pesa yangu yote LEO, na madai yangu ya fidia yapo palepale kwa usumbufu huu wa kikatili.
Majina na mawasiliano yangu nimewapa mods wa JF