Sawa,so kila unapofanya kazi unanyanyaswa thats why hutulii kwenye ajira?
Ngoja nikwambie dogo,inawezekana kabisa ukawa ni mfanyakazi mzuri sana,pia naweza kuwa msaada kwako ingawa unaendekeza dharau,ebu kuwa wazi,nini kinakufanya kuacha/kutopata ajira ya kudumu?manyanyaso gani unafanyiwa?
Kuwa wazi upate msaada.
Sio kila nnapofanya kazi nanyanyaswa, mbunge niliachana nae kutokana na kukaa bench mda mrefu bila kuwa na uhakika wa kipato, kipato ni kukiwa na kazi,
Nikapata kazi mikono speakers nimefanya miezi kumi bila matatizo boss wa kike alipoondoka madaraka akaachiwa bwana DEO hali ikabadilika
Kazin natakiwa kuripot saa mbili lakini boss anataka nimfuate kwake saa moja kamili na gari inalala ofisini.
Dharau, kejeli maongez yake ni kuponda tuu hajawahi kusifia
Mda wa kula unampeleka sehem ambayo mi siwez Ku afford na anakunyima kwenda sehem nyingine kula, hivyo nashinda njaa
Mda wa kaz unaisha ye bado anasafar zake hatak niondoke nitazunguka nae mpaka sa nne usiku gari napaki kwake kesho saa moja niwe nimefika.
Matus mbele za watu, dharau za kila aina kejel na majigambo, ashawahi kunimwagia maji sababu ya kudai haki yangu.
Na mengine mengi tuu. Nkaamua kuacha.
Nkapata kwa jamaa anaitwa ASAD ni raia wa Pakistan nimefanya nae kaz miez 6, kapata kaz nje nchini China miez 6, nikakosa kazi.
Nkaendesha gar ya mtu uber, hali ni mbaya mwenye gari haelewi anataka hesab 40,000 mafuta niweke Mimi, traffic wakiona namba nyeupe ni kikwazo kwao utapigwa mkono kila sehem, mwisho wa siku bila 40 tajir haelewi nakesha usiku mzima kufanya kazi ili nifikishe hesab yake, nimemweleza tajir na kumuomba Mara kadhaa ashushe hesab anaona hela ndogo. Kuliko kugombana au kufika mbali nikaona nimuachie gari yake.
Sina matatzo na mabosi sijapata sehem ya uhakika na mkataba wa kueleweka.
Kama umeelewa nashukuru