Dreamliner ATCL yatumwa Sudan

nikiona wanajeshi mi muda wote Naona kama wako ktk mateso hawana amani,sjui hata kwanini nawaoneaga Huruma!
 


Maafisa na Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya Serikali ya Air Tanzania.

Wamefanya hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.
 
Kufa kufaana, wapigane ndege yetu ipate trip, nimekumbuka ishu ya mahindi!!
 
Hii habari mbona ya kitambo au umetoka leo kwa msamaha wa Rais!
 
That is a charter flight....Atcl itakuwa imekula hela ndefu kama hamna ufahamu na baadhi ya field bora upite kama upepo bila kutoa comment
Kwa hiyo hadi litokee dili jingine la kusafirisha wajeda au minofu ya sangara ndo litaruka, tuliwaambia acheni watu na makampuni binafsi wafanye biashara. mbona serikali ni mwanahisa kwenye makampuni kibao na wala haihusiki moja kwa moja kwenye management?
 
Itarudi na maafisa na askari wa idadi hiyo waliomaza zamu yao huko Dufur
 
Nadhani lipo kwenye taratibu za mwisho kupewa jeshi kama ile ngalawa letu pendwa
 
Linayo na karibu litaanza, sasa hivi "lina-trot" kwanza


Hiyo route ni ya wapi Mkuu maana dege letu halieleweki,linapigwa pigwa picha tu likifanya kasafari kadogo
 
That is a charter flight....Atcl itakuwa imekula hela ndefu kama hamna ufahamu na baadhi ya field bora upite kama upepo bila kutoa comment
Hizo hela ndefu Nani anatoa!!?? Kwani UN hawana bajeti,hawajui Bei ya tikeki ya ndege dar to darfuu,hawajui idadi ya manajeshi wa tz wambao ambao watenda huko.............

Wao wametoa nauli ya ndege kufika darfuu, mitembea/basi/treni/gari binafsi juu yenu, ilimradi mfike darfuu kwa wakati....
 
Sipendi huu msemo "kuunga mkono juhudi" unapotumika hata kama ni kwenye jambo zuri mi huona kama ulaghai tu na kutafuta sifa
 
Linaingiza faida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…