Unataka share nini kiongozi!!!!duh. imelipiwa shi ngapi?
Safi sana. Hongera JPM.
Chadema pingeni basi.
UN watakua wamelipia ,sio mbayaMay 16, 2019
Ndege ya ATCL aina ya Dreamliner yaenda Sudan kupeleka wanajeshi ktk jimbo la Darfur kulinda amani.
Akizungumzia ushiriki wa Tanzania ktk kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa, mkuu wa operesheni ktk JWTZ Major General Alfred Fabian Kapinga amesema huu ni mwaka wa 12 toka Tanzania ihusike ktk kampeni za ulinzi wa amani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.
Tanzania ina vikosi chini ya Umoja wa Mataifa kulinda amani ktk nchi za Lebanon, Central African Republic, Sudan na DR Congo. Na kati kupeleka vikosi imekuwa ikitumia ndege za JWTZ na zingine zilizokidishwa na Umoja wa Mataifa. Hii ni mara ya kwanza ATCL kutumika na kutakuwepo mwendelezo wa ATCL kutumika ktk misheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Asie jua maana, haambiwi maanaNaomba unieleweshe ni kipi cha kumpongeza hapo Magufuli?
Asie jua maana, haambiwi maana
Labda hazijachezewa hapo,wanasema imelipiwa na UNYaani kodi za wananchi ndo zinachezewa hivi, shenzi kabisa
Naomba unieleweshe ni kipi cha kumpongeza hapo Magufuli?
Tulia mkuu! Kama tumelipwa kwa usahihi hamna shida,tuombe waendelee kutupa dili kuliko kuziacha ziozee uwanjani,kila biashara ina risk zake,ikitunguliwa basi ni ajali kazini! Ila labda tu tuambiwe ile 10 percent imeenda kwa nani! Maana ni obviousNdege yetu ikatokea inatunguliwa,lawama kwa nani?! Kwa nini wasipelekwe na ndege za UN ambazo zinatambulika na kisheria haziruhusiwi kushambuliwa?!
Tumekosa safari za kimataifa zenye tija hadi tuvizie mara kupeleka mbuzi Dubai na sasa wanajeshi Sudan?! Je safari hizo ni endelevu kwa wiki ama mwezi mara ngapi?!