Dream of becominng a Mzungu

Kwanini tusiupende utanzania wetu?Mzungu mzungu!Mzunguu kitu gani bwana?huo ni utumwa.
 
Kutokujiamini.....unaamini cha mwingine ni bora kuliko chako. Kimsingi wazungu/watu weupe, I mean pinkish, wangekuwa wanajaribu kutafuta ngozi nyeusi (brownish) wangeeleweka. Maana hivi yetu ni ina kinga zaidi.
Mungu katupenmdelea, then tunaharibu,....pambafu!!!
 
Ndio mambo ya wakina dada zetu wanayapenda haya na kujifanya wazungu kumbe ni Wasukuma wa Mwanza
 
Hata siku moja siwezi kutamani kuwa Mzungu. Nauthamini sana Uafrika wangu na pia kuwathamini Waafrika wenzangu. Kwa maoni yangu ngozi yetu ni ngozi nzuri sana inayoweza kustahamili hali za hewa zote duniani kama vile joto na baridi. Huwa nawashangaa sana Wanaohangaika kujichubua ili wawe na ngozi nyeupe ambayo hawakuzaliwa nao. Black is beauty.
 
Black and proud. Hivi kuwa mzungu ndio nini? Lets be judged by the standards we uphold as colour is just skin deep. Ingekuwa damu yao ni rangi tofauti ningekuwa na wasiwasi. Kumbuka such feelings are inferiority complex and its the worst kind of poison as its colonization of the mind.
 
Wanaharibu rangi nzuri ya kiafrica kisa uzungu na wakibabuka ngozi wanakuwa kama midoli vile.
 
Naomba tusiwahukumu sana hawa ndugu zetu wanaotamani uzungu. nadhani cha msingi hapa ni kujiuliza kwa nini wanatamani uzungu na siyo uafrika?
Waafrika mpaka karne hii tuliyonayo tumeendelea kuwa na serikali za kipumbavu na kishenzi kama za akina mugabe n.k, Tumeendelea kuwa na ujinga wa mawazo na umasikini wa kufikiri kiasi kuwa rasilimali zetu zinaibiwa na kuchotwa kwa msaada wetu na viongozi wetu. Kwa majumuisho ya mambo yote hayo na mengine nisiyoyaandika ndo mtu mweye tafakari zake anatamani kuwa mzungu. Tatizo siyo rangi ila ni jinsi tunavyoishi na tunavyojitawala na kuyakabili maisha hapa duniani. Naomba tusiwalahumu... Tutumie nafasi hizi kujichunguza na kujirekebisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom