Dream Big

Dream Big

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Nina machache ya kuchambua hapa Jf kuhusu hiyo mada yangu Kwa siku ya Leo japo kwa uchache sana.!

Unaweza kujiuliza ni nini dhumuni langu?
lakini jibu la dhumuni hilo ni kushare japo machache tu niliyonayo.

Sisi kama binadamu tumejaliwa kuwa na upeo wa kufikiri,akili na ata kuchukua maamuzi,.

Wengi wetu tukiwa kwenye umri furani tunakuwa na ndoto au uwezo wa kudream Big na ndoto hizo ndizo zinazotufanya kuchukua hatua furani ili kuzifikia.

Lakini tunapokuwa na hizo ndoto tunasahau kwamba ili utimize ndoto hizo inabidi pia huwe na huwezo wa kuwaza matokeo Chanya ya hizo ndoto.

Ukitaka kuwa na utajiri au kusimamia kile unachokiamini kwa maendeleo yako ya Leo na baadae basi ni lazima ucheze na maneno hayo.

Cha kwanza unatakiwa kufanya yafuatayo;

1: kuamini ndoto zako ndio njia ya mafanikio yako usiende nje ya Ndoto zako.

2:kutekeleza Ndoto zako pasi na kukata tamaa .

3: Mafanikio yako lazima yaje na mitihani ya kimaisha cha kufanya ni kusonga mbele .

4:Hakuna binadamu atakayefurahia maendeleo yako cha muhimu ni kuchukulia Ongera zao kwako kama Changamoto za kutaka kukurudisha Nyuma.

5:Simamia unachokiamini haijarishi ni kwa gharama kiasi gani..!

6:Usifikirie kwamba Elimu ya darasani ndio njia pekee ya kuweza kufanya ukatimiza ndoto zako:

Hapo nielezee kidogo Elimu ya darasani kivipi?
Wengi wanashindwa kutimiza ndoto zao ni kwa sababu tu ya kuamini Elimu ya darasani ndio kila kitu lakini wanasahau kwamba kuna Elimu nje ya darasa
Mfano.
Kusoma vitabu na majarida mbalimbali na kujifunza kwa waliofanikiwa.

Kuna mengi ya kufanya ili utimize ndoto lakini kutokana na Mitihani ya kidunia watu wengi wamejikuta wanashindwa kutimiza Azma ya ndoto zao hivyo ndoto hubaki ndoto mpaka siku ya kifo.

Nb;DREAM BIG.
 
Back
Top Bottom