MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 496
- 768
Mahakama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasilisha rasmi malalamiko katika Bunge la Kitaifa likitaka kuondolewa kinga kwa Constant Mutamba, Waziri wa Sheria ili apandishwe kizimbani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ombi hili linalenga kuruhusu kufunguliwa kwa mashauri ya kisheria dhidi ya Waziri huyo anayetuhumiwa kuhusika na kesi ya utakatishaji fedha ambayo kiasi chake kinatajwa kuwa ni Mamilioni ya fedha.
Mashtaka hayo yanakuja baada ya kuzuiliwa kwa muamala uliotiliwa shaka wa Dola Milioni 19 Mwezi Aprili mwaka jana na CENAREF ukilengwa kwa akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina la kampuni ya Zion Construction.
Ikiwa Bunge la Kitaifa litakubali ombi la Mwendesha Mashtaka, Constant Mutamba anaweza kukamatwa siku zijazo. Mashtaka mahususi bado hayajafichuliwa rasmi, lakini ushahidi mpya unapendekeza kesi inayoweza kumtia hatiani.