Drama la Butiku na Msekwa

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Butiku alinukuliwa akisema CCM haina dira wala mwelekeo kutokana na viongozi wake kuzama kwenye vitendo vya rushwa.

Katika kujibu hoja hiyo Msekwa amesema: “Kuporomoka kwa maadili dhidi ya viongozi wetu si chama kukosa mwelekeo, hayo ni matatizo ya viongozi wetu lakini chama kina dira.”

Msekwa amesema, tatizo ndani ya chama hicho ni kamati za maadili za chama hicho kushindwa kutimiza wajibu wao.

“Unategemea nini kama kamati za maadili zimelala, hizi hazitimizi wajibu wake hivyo vitendo vya rushwa kuendelea kushamiri…ndio maana wananchi wamekuwa na hasira dhidi ya chama chetu,” alisema Msekwa.

My take:
Msekwa anaposema tatizo ni kamati za maadili ana maana gani wakati yeye pia alikuwa kwenye kamati ya Mwinyi iliyoshindwa kusuluhisha makundi ndani ya CCM, au tusema anapingana na maamuzi ya kamati yake.

Mimi nafikiri hii ni comedy mpya baada ya ile ya UVCCM vs NEC-CCM kuhusu malipo ya Dowans na January vs Ngeleja kuhusu kukodi mitambo.
 
Back
Top Bottom