GedsellianTz
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 1,348
- 1,805
1) Nimekuwa Mbunge miaka 15. Ninafahamu msingi 10% ya Mapato ya Halmashauri kutolewa kwa mikopo kwa Wanawake na Vijana. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa haihusiki kwa lolote. Mkuu wa Mkoa hupewa katika Bajeti ya Mkoa Tsh.10Millioni kusaidia miradi ya Wananchi pale anapokuwa na ziara mbalimbali. Mamilioni yanayosemwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa ni uwongo na upotoshaji uliokithiri.
2) Fedha za Mikopo kwa Makundi ya Wanawake na Vijana ni Rebolving Fund, ambayo inasimamiwa na Halmashauri husika. Mchakato, tangu kuchambua, kuwapa elimu, kuwafuatilia hadi fedha kurudishwa ni kazi ya Halmashauri husika kupitia Idara husika ya Halmashauri.
Mkuu wa Mkoa hahusiki. Ni Wehu na kuingiza siasa mahali pasipostahili kwa kuwa matokeo yake ni kufanya hizo fedha zisiweze kurudishwa.
Nimekutana sana na matukio ya aina hiyo wakati nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa.
Aidha, Halmashauri ambazo nazo zilikuwa hazitengi fedha hizo asilimia 10% Watendaji wake tulikuwa tukiwapiga wao wenyewe faini. Hivyo Mrisho Gambo asiwapotoshe Watanzania. Vita vyake na Lema isije ikaathiri utendaji kazi wa mifumo ya Serikali iliyowekwa siku nyingi.
Mpango huo wa kuzitaka Halmashauri kutenga fedha ulianza Wakati Kingunge Ngombale Mwiru akiwa Waziri wa TAMISEMI. Propaganda anazofanya Mrisho Gambo ni za kitoto sana, bahati mbaya katika nchi hii ninajua mengi, na hakuna wa kunidanganya. Hivyo, mbuyu uitwe tu mbuyu. Huu mchezo anaofanya Mrisho Gambo ndio unaozidi kupandisha watu hasira kama alivyotaka kufanya wakati wa Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto.
3) Meya, sikutetei kwa kuwa ni Halmashauri ya Chadema. Ninasimamia ukweli. Wananchi wa Arusha sio wote wa Chadema. Hata wasio Chadema wanahaki na fedha hizo kwa kuwa wote walipiga kura na hivyo wote wana haki ya kunufaika na kura zao. Meya, chapa kazi bila ubaguzi wa aina yeyote. Simamia ukweli, simama penye haki, Mungu atabariki, lakini usikubali laana ya ubaguzi kwa kuwa unashindana na huyo ambaye hajui mipaka yake ya kazi.
4) Fedha 10% za Halmashauri zinaongezewa pia fedha kutoka Hazina kupitia kinachoitwa " Fidia ya vyanzo vya usumbufu". Hizo ndizo nadhani Mrisho Gambo anaziita fedha za TAMISEMI. Wizara ya Tamisemi kama msimamizi wa Serikali za Mitaa, ni daraja tu, lakini fedha za fidia zinaidhinishwa na Bunge la JMT kwa lengo la kuzirudishia Halmashauri fedha kutoka vyanzo ambavyo 2002 vilichukuliwa na Serikali Kuu. Ninavyoelewa hakuna utaratibu mwingine uliofanyika. Hivyo hizo fefha ni kodi ya Watanzana wote na Mrisho Gambo hana haki yoyote ile ya kuzifanyia Propaganda za Kisiasa.
Manispaa ya Arusha tembeeni kifua mbele kutimiza ahadi yenu, na ninaziomba mamla zote za Halmashauri zitimise ahadi zao ili Watanzania wote bila kujali itikadi zao wanufaike. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu wabariki Wanyofu wa moyo wanaotekeleza majukumu yao kwa kadiri ya mapenzi yako na siyo matakwa binafsi ta mtu mmoja mmoja.