Dr. Vicent Mashindi Bawacha Jiandaeni kwenye Mandalizi ya Miaka 25 ya CHADEMA

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,249
2,000
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vincent Mashinji akiongea na viongozi wa kichama ngazi ya chini Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Kata ya Lugarawa.

Dr. Mashinji amewataka viongozi hao kusahau yaliyopita na sasa kujipanga kikamilifu kuimarisha Chama na kutafuta wananchi wenye sifa za uongozi ili waweze kuwashawishi waje kugombea nafasi mbalimbali za Serikali na kwa kuanzia uchaguzi mdogo wa 2019 kugombea wenyeviti wa serikali za mtaa na 2020 udiwani, na Ubunge.

“kwa kufanya hivyo tutaweza kupata watu makini na wanaopendwa na wananchi hali amabyo itaisaidia Chama chetu kutokuwepo na migogoro ya uteuzi wa viongozi, na kuhakikisha watu hao ni watu wanaofanya shughuli na Chama na kushiriki shughuli za kijamii ili itusaidie kuimarisha Chama chetu sehemu husika na kutupatia wanachama wengi zaidi watakao weza kutupatia ushindi Chama chetu na kulikomboa Taifa hili”

“Niwaombe viongoze wetu wa Chama Jimbo la Ludewa yenye jumla ya kata 27 na vijiji 77 kutumia njia mbalimbali kuwaeleza wananchi uovu wa Serikali iliypo madarakani na kuwashawishi kwa kuwaeleza ni Chama gani kitakacho wapatia huduma zao za msingi,kwa kutumia rasilimali zilizopo Ludewa kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia vyeme Mgodi wa makaa ya mawe(Mgodi wa Mchuchuma),Mgodi wa chuma ( Mgodi wa Liganga) na machimbo ya dhahabu (Amani) amapo umbali wa kutoka Mgodi wa Liganga mpaka Mgodi wa Mchuchuma km 60 lakini 50 ya uhuru bado Ludewa imekuwa ni sehemu mojawapo iliyokosa maendeleo” Alisema Dr. Vincent Mashinji

Dr. Vincent Mashinji alitumia kikao hicho kuwataka Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Tanzania nzima kufanya maandalizi ya kuazimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mwaka kesho, na kuwaahidi Baraza hilo kwenda kulipigania kwenye vikao vya Kamati Kuu vitakavyokaa ili liweze kuwapatia wanawake nafasi hiyo ya kufanya maandalizi hayo.

Shere ambayo Tanzania na Dinia nzima itatambua kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetizima miaka 25 kwa kuwatumikia watanzania na kuwapigania haki mablimbali na wananchi.

Kwa kufanya hivyo Chama kinatambua umuhimu mkubwa wa Mabara yake ikiwemo Baraza la Vijana Chadema pamoja na Baraza la Wazee Chadema lakini kuwapa jukumu Baraza la Wanawake jukumu hilo kubwa la kufanya maandalizi hiyo ni kwasababu kuwa na imani kubwa na wanawake kufanya vizuri pale ambapo wanapopewa jukumu la kulitekeleza.

Dr. Mashinji aliwataka wanawake kuungana kikamilifu ili kuweza kuleta maendeleo kwa jamii nzima kwa kushiriki na kufanya shughuli za kijamii na kukipigania Chama chao, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutimiza msemo wao wa kusema Wanawake ni chimbuko la Maendeleo.

Dr. Vicent Mashinji aliyasema hayo wakati akiongea na viongozi wa Chama kuanzia ngazi ya chini ya Chama kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika Kata Lugarawa iliyopo Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom